Sunday, July 25, 2021

Fahamu njia 10 za kuwa masikini










Habari yako msomaji wa makala hii, natumai umzima wa afya na waendelea vyema. Leo  nimeleta mada hii kwenu kwa sababu wengi wetu tunahamasika au tunasikiliza habari mbalimbali juu ya kuwa tajiri tu Jambo ambalo kwa namna moja ama nyingine huwezi kufikia Kama hujui vitu vitakavyo tufanya uwe masikini. Nimekuletea dondoo 10 muhimu za jinsi ya kuwa masikini kwa haraka shuka nazo πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

1.Usiamke mapema.

Watu wengi wamekuwa na mazoea ya kutoamka mapema wakiamini hate wakifanya hivyo hawana Cha kufanya, lakini ukweli ni kwamba kuwa na mazoea ya kuamka mapema kutakufanya uwe mchangamfu na pia hate ikitokea umepata kazi itakuwa rahisi kwako kuweka uaminifu kazini kwa kufika mapema. Jaribu kuamka mapema Kila siku halafu uwaze Jambo jipya la kufanya ambalo ni tofauti na ulilofanya jana hi itasidia uwe na mawazo angavu.

2. Usipange matumizi ya Pesa zako.

Watu wengi tunaamini kuwa matumuzi hayawezi kufanyika hadi uwe na pesa lakini kiuhalisia inabidi upange matumizi kwa mfano, kama unaishi peke yako inabidi ukadirie kiasi gani cha pesa unatumia kwa siku na hata wakati mwingine tumia chini ya hicho kiwango kuangalia upungufu utakaojitokeza hii itakupa ujasiri wa kuishi na kufanya mambo yako bila shida yoyote.  


3. Usiweke akiba mpaka utakapo-kuwa tajiri.

Akiba ni nguzo muhimu ya mafanikio asikwambie mtu kwamba akiba ni kwa ajili ya matajiri tu. Hali hii inaonekana sana katika familia na jamii yetu ya watu wa chini kuweka akiba ni sawa na kujipendekeza katika utajiri, ni kweli kwamba hakuna mtu aliyezaliwa tajiri ila inabidi tujipendekeze kupiga hatua fulani ya mafanikio. Zipo njia nyingi za kuweka pesa zako Kama vile benki, kutunza kwenye simu na pia hata kwenye kibubu.

4. Chagua kazi. Mimi nimesoma siwezi kufanya hii kazi. Usikubali kazi zisizo za hadhi yako!

Vijana tulio wengi hususani wasomi tunatabia ya kuchagua kazi jambo ambalo linatufanya tukose vigezo vya kushiriki na wanajamii wengine . Mbinu moja ya kufanikiwa ni kufanya kazi yoyote ile ya halali kwako na pia uepuke kazi zitakazo kufanya usiwe huru Kama vile, uuzaji wa bangi au madawa ya kulevya ijapokuwa kazi hii inalipa lakini sio nzuri kuifanya kwa kuwa inaenda kinyume na sheria ya nchi.

5. Usifikirie kuanzisha biashara mpaka malaika akishuka kutoka mbinguni na kukukabidhi mtaji wa kueleweka.

Katika suala hili vijan tulio wengi tumekuwa watu wa kutaka kushauriwa juu ya biashra ya kufanya ewe kijana mwenzangu panga biashara yako kichwani Kisha upate watu sahihi was kukushauri juu ya biashara yako na sio kwenda kwa watu kutafuta mawazo juu ya biashara ya kufanya utakosa ujasiri (confidence) katika hiyo biashara.

6. Endelea kuilaumu serikali na wazazi ambao hawakukupa Elimu. Laumu wote ambao unahisi wana hela na ni wachoyo hawataki kukupa.


7. Tumia Pesa nyingi kuliko kipato chako.

Vijan wengi tumezoea kutumia pesa nyingi kuliko tunazopata na hii imesababisha badala ya kuongeza bali tuanapunguza. Kwa mfano, Unaweza mkuta kijana anapata 50,000/= kwa wiki lakini anahitaji Kila wiki atumie 100,000/= kwenda kwenye kumbi za starehe n.k

8. Hakikisha unaenda na fashion. Kila toleo jipya la nguo, viatu, simu lazima na wewe ununue. Kila harusi hakikisha unavaa sare na umependeza mpaka wakukome.


9. Wanunulie watoto wako chochote watakacho kuomba ili waone unawapenda sana.


10. Endelea kutumia muda mwingi zaidi kwenye social networks. Kama Whatsapp, Facebook na Instagram negatively, sengenya wote wanaopiga hatua maana ni freemason hao. Kaa nao mbali kabisaπŸ™

Watu tulio wengi htujui matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii na hivyo kupoteza muda katika kuangalia katoon, video miziki  na kupoteza muda bila mafanikio. Mitando ya kijamii Kama YouTube, Instagram, Facebook  sio kwa ajili ya kuposti picha Kama watu wengi tunavyofanya lakini Ni miongoni mwa njia za kupata ajira, kupitia mitandao ya kijamii unaweza kufanya yafuatayo;

Kutangaza biashara yako online au biashara ya kampuni 

Kuwa muhamasishaji wa mitandao ya kijamii - influencer

Pia Kuna mitandao ya kuuza picha, yaan kazi yako kutafuta location nzuri unapiga picha unatuma hivyo utalipwa kupitia watu watakavyoinunua

Pia unaweza anzisha blogs au website ambayo utalipwa kupitia Ads kutoka Google AdSense

Pia kupitia Whatsapp unaweza kuposti bidhaa zako na si Kama watu wengi wanavyofanya kujipost wao wenyewe. Simaanishi kwamba ni vibaya lakini walioweka status bar walikuwa na matarajio makubwa juu ya watumuaji na si hivyo tunavyofanya.

Asante, San kwa muda wako

Dr, kwayu.

UDSM -Duce



No comments:

Featured Post

 SOMA SIMULIZI ZENYE KUSISIMUA HAPA A. UTAJIRI WENYE UCHUNGU     UTAJIRI WENYE UCHUNGU-1     UTAJIRI WENYE UCHUNGU-2      UTAJIRI WENYE UCH...