SWALI : Kwa kutumia mifano kuntu onesha fonolojia arudhi inavyojitokeza katika lugha
ya Kiswahili huku ukionesha uamilifu wa kila kipengele
Fonolojia
arudhi,(Mgullu 2010),ni tawi linaloshugulikia maswala mengine ya sauti ambayo huathiri
vipashio vikubwa zaidi kuliko fonimu moja, pia huchunguza namna ya kuweka mkazo
katika maneno na tungo katika lugha fulani kama vile kiimbo na muundo wa
silabi. Fonolojia arudhi ya Kiswahili huchunguza sifa za kiarudhi ambazo huathili vipashio vikubwa
kuliko fonimu na alofoni zake.
Kiujumla fonolojia arudhi ni tawi linalochunguza sifa za kiarudhi ambazo
huathiri vipashio vikubwa kuliko fonimu na alofoni zake.Katika lugha ya
Kiswahili fonolojia arudhi inajitokeza kwa namna mbalimbali kama ifuatavyo;
Lafudhi,
ni sifa ya kimasikizi inayohusiana na kusikika kwa sauti wakati wa kutamkwa na
msemaji binafsi ambayo humpa utambulisho wa kijamii(kijiografia). Lafudhi ni
athari ya lugha ya kwanza kwa lugha ya pili, na kwakuwa lugha ni zao la jamii huwa
na mazingira yake ya kijiografia au kieneo inamopatikana, ndio maana suala la
mazingira ya kijiografia limehusishwa na lafudhi mfano,
Nakwenda
kurara badala ya kulala ( mkurya)
Fyatu
fyangu fimeharibika ( mnyakyusa)
Ntoto
nchanga analia( mmakonde)
Katika lugha ya Kiswahili lafudhi ina uamilifu wa
kuonesha sehemu ambapo mtu anatoka, mazingira alimo au lugha yake ya kwanza,
athari ya lafudhi sio lazima iwe athari ya lugha mama kwa lugha ya pili pia
inaweza kuwa athari ya lugha zinazomzunguka
mtu.
Wakaa,
ni mda unaotumika wakati wa utamkaji wa sauti au silabi,kuna baadhi ya
wazungumzaji wanaweza kutambulishwa lafudhi yao kutokana na uvutaji au
urefushaji wa sauti. Mfano wabena wakiwa wanauliza swali husema,
Mfano(a) kwani huyu mtoto ni wan:ani,?
yeye ni mt:oto?
Pia katika lugha ya Kiswahili wakaa hujitokeza
katika idadi ya maneno kadhaa ambayo ni;
Mfano(b) Majini(mashetani) _
m:ajini(ndani ya maji)
Wake (wanawake walioolewa) _
w:ake(umiliki)
Uamilifu wa wakaa katika lugha ya kiswahili ni
kuonesha tofauti ya maana baana ya maneno,
pia husaidia kubaini lafudhi ya mzungumzaji mfano wabena kwenye mfano(a)
hapo juu.
Kidatu,
ni kiwango cha sauti kinachosikika wakati wa utamkaji wa maneno. Kidatu ni sifa
ya msikiko wa sauti ambayo humwezesha msemaji kubadili kiwango chake cha sauti
kwanzia chini kati hadi juu bila kijali kasi ya mawimbi yake anayoyatoa, katika
lugha ya Kiswahili kuna aina tatu za vidatu kuna kidatu juu, kati na chini kwamfano.
‘Njoo
Njoo
‘ˉNjoo
Uamilifu wake katika jamii ni kupamba lugha,
husaidia kutumia lugha kulingana na mazingira na hetegemea zaidi uhusiano wa
wazungumzaji.
Kiimbo,
ni umbo la sauti linalotokana na mpando-mshuko wa sauti za lugha wakati wa usemaji.
kila lugha ina utaratibu wake wa kupanda na kushuka kwa mawimbi sauti lakini
katika lugha ya Kiswahili kiimbo kimegawanyika katika makundi manne ambayo ni;
(a)kiimbo maelezo – hutoa maelezo, mfano; amefika
leo asubuhi kutoka safari.
(b)kiimbo swali
- kuuliza swali, mfano; kwanini hujaja?
(c)kiimbo amri
- kuamuru, mfano; njoo haraka
(d)kiimbo mshangao – kushangaa, mfano; amekufa !
kiimbo katika
lugha ya Kiswahili huwa na uamilifu wa kubaini lengo la msemaji kama vile
kuuliza maswali, kuamuru, kutoa maelezo na kushangaa, kwa kurejelea mfano hapo
juu (a-d), pia husaidia kuonesha hisia za msemaji na hali mbalimbali kama vile
hali ya masharti, mazoea, uyakinifu na ukanushi
Mkazo,
Ni nguvu inayotumika wakati wa utamkaji
wa sauti za lugha, kila lugha huwa na utaratibu wake wa ujitokezaji wa mkazo
lakinikatika lugha ya Kiswahili mkazo hutokea katika silabi ya pili kutoka
mwishoni upande wa kushoto mwa neno. Wasemaji wa Kiswahili sanifu walioathiriwa
na matamshi ya lugha ya kiarabu huwa wanaweka mkazo katika silabi ya kwanza au
ya pili badala ya silabi ya mwisho kasoro moja kama ilivyo kawaida ya utamkaji
wa maneno ya Kiswahili sanifu, Huonesha kwamba katika lugha ya kiarabu maneno
huwa na mkazo katika silabi ya kwanza au ya pili ya neno.
Mfano(a) Fa′hamu badala ya faha′mu
Mu′stafa badala ya musta′fa
Kuba′riki badala ya kubari′ki
Mfano(b) Ba′rabara (njia)
Bara′bara(sawasawa)
Uamilifu wa kiimbo katika lugha ya Kiswahili ni
kuonesha utofauti wa maana za maneno kulingana na mkazo wa sauti.
Hitimisho,Vipengele arudhi hupatikana katika lugha
zote za mwanadamu ijapokuwa kuna baadhi hupungua kwa baadhi ya lugha mfano
katika lugha ya Kiswahili na kinyakyusa kipengele arudhi cha toni hakipo. Pia
kukosekana kwake katika lugha husababisha kutokea kwa utata katika maneno au
neno ya lugha husika.
MAREJEREO
Massamba, D, KihoreY na MsanjilaY, (2004), Fonolojia
ya Kiswahili sanifu. TUKI: Dar es salaam.
Mgullu, R.S.(2010). Mtaala wa isimu: Fonetiki,
Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili. Nairobi:Phoenix.
TUKI(2004) Kamusi ya Kiswahili sanifu. Dar ea
salaam: TUKI.
No comments:
Post a Comment