SWALI :Fafanua dhana ya uziada katika
taaluma ya fonolojia, toa mifano katika lugha ya kiswahili.
Uziada, ni kuwepo au kutokuwepo kwa sifa fulani
kutokana na kutabirika kuwepo au kutokuwepo kwa sifa nyingine. Hususani zile
ambazo si muhimu kubainisha fonimu (Andrew Nyaga 2017).
Uziada, ni utabirifu wa sifa ambazo ingawa ni
kijenzi cha kipande sauti lakini si muhimu katika fonolojia ya lugha husika.
Uziada umegawanyika katika namna kuu mbili nazo ni; uziada katika vitamkwa
ambapo hutokea pale ambapo ukijua sifa fulani za kipande sauti unaweza kutabiri
sifa nyingine zinazoendana na sifa hiyo, na huonesha mashariti zuizi ya sifa za
vitamkwa/ vipande sauti ambayo hueleza kwamba kama kipande sauti kimoja
hakiwezi kuwa na sifa mbili zinazokinzana, pia uziada mwingine hutokea katika
mpangilio wa vipande sauti katika kuunda maneno ambapo mfuatano wa sauti
huweka mashariti zuizi katika mfuatano
wa sauti, mfano katika lugha ya kiswahili hakuna mfuatano wa konsonanti nne(4).
Uziada unaweza ukajidhihirisha katika vipengele mbalimbali au sifa mbalimbali
kama ifuatavyo;
Sifa bainifu kwa kigezo cha mkondo hewa, katika
kigezo cha mkondo hewa kitamkwa kinatolewa kwa kuzingatia chemba ambapo ala
tuli na ala sogezi hukutana au chemba inayohusika na utamkaji wa sifa fulani.
Sifa za ziada tunazozipata katokana na kigezo hiki ni kama vile +korona, anteria,
midomo, meno, glota na tawanyifu.
+kons +kons +kons
+mido -kor +ante
-Naz +mido +meno
-Tawa +naz -tawa
-kor -tawa -mido
-glota
+kor
Sifa bainifu zinazohusu kiwiliwili cha ulimi, katika
kigezo hiki vitamkwa hutolewa kwa kuzingatia mkao wa ulimi wakati wa utamkaji
ambapo ulimi huweza kuinuliwa juu kabisa kwenye chemba ya kinywa au kutamkwa wakati
ulimi umelala chini kabisa na kiwiliwili cha ulimi kikiwa kimerudishwa nyuma
kiasi.Sifa bainifu tunazopata kaitika kigezo hiki ni juu, uchini na unyuma.
Mfano.
+kons +kons +sila
+juu +juu +chini
+nyuma +nyuma -juu
-chini -chini -nyuma
Sifa bainifu zinazotokana na namna au jinsi ya
utamkaji, Katika kigezo hiki sauti ambazo wakati wa utamkaji wake huruhusu
kongomeo kurindima kwa nyuzi sauti hubainisha vitamkwa ambavyo hutamkwa wakati
mkondo hewa unatiririka bila kizuizi kikubwa pia inahusu sauti ambazo wakati wa
utamkaji wake ulimi huzuia mkondo hewa usipite katikati ya kinywa bali pembeni
mwa ulimi katika pande zote mbili, pia sifa hii inahusu sauti zote ambazo
hutamkwa kwa kushusha kidakatonge na kuruhusu mkondo hewa upite puani badala ya
kinywani. Hata hivyo sifa hii hulazimisha utamkaji ambao hewa kupitia katikati
ya sehemu mbili kiasi kwamba hutoa sauti yenye mtikisiko mkali. Aidha sifa hii
hutusaidia katika kutofautisha sauti zilizo katika kundi moja, kupitia kigezo
hiki tunapata sifa za uziada kamavile ghuna, kontinuanti, tambaza, ustridenti,
viringe.
Mfano.
+kons +kons +kons
+ghuna +tamba +kor
-kor -kont -naza
-kont -naza -tamba
-tamba -stride +stride
-naza -viri -viri
-stride
-viri
Iktisadi na uziada katika sifa bainifu, katika
utumiaji wa sifa bainifu inafaa kutumia sifa muhimu tu katika kuainisha
kitamkwa fulani na zile za ziada au zinazotabirika ziachwe kwa hiyo iktisadi ni
kanuni inayohitaji vigezo vichache au mambo machache yanayoweza kuelezea mambo
mengi. Hii inamaana kuwa katika utumiaji wa sifa hizi bainifu inafaa kutumia
sifa muhimu tu katika kubainisha kitamkwa fulani ingawa kitamkwa kinaweza kuwa
na sifa nyingi sana.
Mfano.
+kons
-sila
-ghuna
+mido
+anti
-kont
- Naza
-Tamba
-Koro
Sifa
hizi kwa kutaja chache zinajumuisha na sifa za ziada ambazo hazina umuhimu
wowote , tukichunguza sifa za muhimu tu tunapata.
Mfano.
+ante +naza
-kor +mido
+ante
+ghuna
-sila
+kor
Pia
tunapata sifa chache ambazo ni;
/m/
+ante
-kor
Uziada beleshi, hii ni sifa inayotabilika kwa
kuangalia sifa zingine zenye umuhimu kifonolojia. Hivyo kuna sifa bainifu za
ziada zinazoweza kutabilika ingawa hazipo , sifa hizi huondolewa kwa kutokuwepo kwa sifa fulani kutabilika
kutokana na kuwepo au kutokuwepo kwa sifa nyingine. Kwamfano [+sila] sawa na
[-kons]. Kwahiyo [+kons] ni uziada kama umetumia [+sila], katika kubainisha
sifa bainifu kuna uziada wa sifa zisizowezekana.
Mfano.
+juu
Ila[
+juu, -chini] inawezekana ingawa [-chini] ni uziada
Mfano.
Nazali zote ni ghuna kwahiyo kuweka sifa
ya [+ghuna] au [+kons] ni ziada tu kwakuwa zinatabilika kama vile.
+naz +naz
+ghuna -sila
-son badala ya +ante
+kons -koro
-kont
Kinachotokea
ni uwili unaokinzani, ambapo sifa moja ikitolewa hamna haja ya kutoa sifa
nyingine.
+sila -kons
+ghuna = -ghuna
-juu +chini
Ujumuisho
ambao sifa moja inajumuisha sifa nyingine.
Mfano
+naza
- ghuna
Pia
katika suala la mantiki.
-Juu hivyo tafisri yake ni [+kati]
-Chini
Hitimisho, katika lugha ya kiswahili uziada katika fonolojia
hutusaidia kubaini sifa bainifu za vitamkwa vya lugha mfano kama sauti ni ghuna
hutusaidia kujua kuwa sauti hiyo sio ghuna, pia kama sauti ni kipasuo husaidia
kubaini kuwa sauti hiyo sio fulizwa japo sio mara zote kwani kuna wakati ukijua
sifa ya sauti fulani thamani ya kitamkwa hicho inaweza kutupa taarifa za ziada
kuliko thamani ya sifa hiyo ambayo ni kinyume chake.
MAREJELEO
Chomsky,
N .&
Halle, M (1968). The sound pattern of English .New York Harper&
Row.
Massamba,
D.P.B (2012) Misingi ya fonolojia.Dar es salaam:TATAKI.
Massamba,
D.P.B, (2011) Maendeleo katika nadharia ya fonolojia.Dar es salaam: TATAKI.
Inew
mgaya. Blogspof. Com.