SWALI: Fasihi ya Kiswahili imekuwa ikibadilika sambamba na mabadiliko ya jamii husika .Jadili kauli hiyo kwa mifano maridhawa kutoka katika riwaya ya Kiswahili
Fasihi imejadiliwa katika mitazamo mbalimbali mfano ule unaodai kuwa
fasihi “literature” ni jumla ya maandishi yote katika lugha Fulani,( Wallek na
Warren 1986:20).Mtazamo mwingine ni ule unaodai kuwa “literature” au fasihi ni
maandishi bora au jamii ya kisanaa yenye manufaa ya kudumu (H. Summers
1989:357). Pia mtazamo uliozuka hapa Afrika Mashariki na kuenea zaidi miaka ya
1970 ni ule unaosema kuwa “Fasihi ni hisi ambao unafafanua kwa njia ya lugha
(Ramadhani J.A 2:6)”.Hivyo kwa ujumla Fasihi ni utanzu au tawi la sanaa ambalo
hutumia lugha hutumia lugha ya mazungumzo au ya maandishi ili kufikisha ujumbe
kwa hadhira husika.
Fasihi ya Kiswahili,pia imejadiliwa na
wataalamu mbalimbali,mfano (Syambo na Mazrui 1992), anjadili fasihi ya
Kiswahili kuwa, ni ile inayoandikwa kwa kiswhili tu,iwapo inazungumzia
utamaduni wa Kiswahili au utamaduni mwingineo maadamu fasihi hiyo imetumia
lugha ya Kiswahili na imefuata mbinu za ufasaha wa lugha hiyo. Mabadiliko, ni
hali ya kutoka hatua moja kenda nyingine ,mabadiliko hayo yanaweza kuwa chanya
au hasi. Fasihi ni zao la jamii hivyo haina budi kubadilika kulingana na
jamii.Riwaya kama kazi moja ya fasihi ni hadithi ndefu ya kubuni yenye visa
vingi, wahusika zaidi ya mmoja yenye maelezo na mazungumzo yanayozingatia kwa
undani na kwa upana zaidi.Ni kweli kwamba fasihi ya Kiswahili imekuwa
ikibadilika sambamba na mabadiliko ya jamii,mabadiliko hayo yako katika vipindi
mbalimbali kama ifuatavyo;
Kipndi kabla ya uhuru, Hiki ni kipindi
ambacho jamii iliishi chini ya utawala wa wakoloni ambapo watu walinyanyaswa,
walikosa kukosa haki, walikandamizwa kutokana na utawala wa mabavu wa
wakoloni.Katika kipindi hiki kuliandikwa riwaya maarufu inayoitwa “Uhuru wa watumwa” ambayo iliandikwa na “James
Mbotela” (1934) ambayo ilikuwa ni zao la mashindano yaliyoendeshwa na kamati ya
Kiswahili ya Afrika mashariki mwaka 1930 na kuwa riwaya ya kwanza ya Kiswahili
,riwaya hii iliandikwa kuonyesha ushenzi uliokuwa ukifanywa na Waarabu,
Waswahili, na Waislamu ambao walikuwa wakiendesha biashara ya utumwa na
kuwachora , kuwakweza waingereza kwa kuwaona kama wakombozi walioletwa na Mungu
kukemea ukandamizaji huo.Hivyo riwaya hii iliandikwa kutokubaliana na utumwa ,
uovu, au uonevu uliokuwa ukifanywa na waarabu.
Kipindi baada ya uhuru, Hiki ni kipindi
ambacho jamii iliishi kwa kutaka uhuru wa kweli
ambapo wananchi walitegemea uhuru wa kweli na ujenzi wa jamii mpya na
ukombozi, ambapo viongozi baada ya uhuru baadhi walikuwa wakiendeleza kasumba
za ukoloni kwa kutowajali wananchi ambapo jamii ilijaa manyanyaso, matabaka ,
ukandamizaji na ubadhilifu wa mali za umma. Hivyo riwaya nyingi zilitungwa kusuta
usaliti huo uliofanywa na viongozi wa kiafrika ili kuweza kujenga jamii mpya
yenye usawa , haki na uhuru. Katika kipindi hiki riwaya za “Shaaban Robert”
ziliandikwa kusuta usaliti huo mfano wa riwaya ni Siku ya watenzi wote
kilichoandikwa na “Shaaban Robert” mwaka (1960-62), riwaya hii
iliandikwa kusuta usaliti uliofanywa na viongozi kwa raia wao.Riwaya hii
inasadifu kabisa mabadiliko katika kipindi hicho, kwani ni kweli viongozi
waliwasaliti wananchi wake.
Kipindi cha azimio la Arusha,Hiki ni kipindi
ambacho ilikusudiwa kujenga misingi ya ujamaa na kujitegemea, Katika kipindi
hiki kuliibuka ujamaa uliolenga umoja na mshikamano, haki na usawa pia, vijiji
vya ujamaa vilianzishwa ili kuhimiza mshikamano huo. Ziiliandikwa riwaya
zilizokuwa zikihimiza umoja na mshikamano mfano wa riwaya iliyokuwa inalenga
kuhimiza huo ilikuwa “Mtu ni utu” kilichoandikw
na( Mhina G, 1971). Hivyo mabadiliko
ya jamii katika kipindi hiki yalisababisha pia kuibuka kwa dhamira ya ujenzi wa
jamii mpya ili kuhimiza mabadiliko hayo.
Kipindi baada ya ujamaa, Baada ya ujamaa
kuliibuka mabadiliko yaliyosababisha kuanguka kwa ujamaa ambayo yalienda
sambamba na anguko la uchumi, ambapo jamii ya wakati huu ilianza kuishi maisha
magumu tofauti na matarajio yao yaliyolengwa na azimio la Arusha, watu walikata
tamaa,walipoteza matumaini.Hvyo riwaya zikaandikwa kueleza anguko hilo kwa
kushindwa kukidhi matarajio yaliyolengwa ,ziliandikwa riwaya zinazoonyesha kuwa
zinausuta mfumo huo wa ujanaa.Mfano wa riwaya ni “Kaptula la Marx” kilichoandikwa na “Euphrase Kezilabahi” ambapo
kiliongelea kuwa viongozi waliiga mfumo ambao hawakuwa na uwezo wa kuutekeleza
na ndio maana Kezilahabi akaandika na kusema “Mtazunguka wee lakini mtarudi
palepale” hii ilikuwa ni kusuta kuwa hawakuwa na uwezo wa kuendana na mfumo
huo. Vilevilie kitabu kingine kilichoandikwa na Euphrase Kezilahabi kinaitwa
“Nyota ya huzuni” ambacho kiliandikwa kuonyesha kufifia kwa matumaini, yaani
yale waliyolenga kuyafikia katika kipindi hicho cha ujamaa yalionekana
kutofanikiwa.Vitabu hivi viliandikwa kwa mafumbo sana ili kukwepa rungu la
tabaka tawala ,mfano kitabu chake Euphrase Kezilahabi cha “Kaptula la marx”.Hivyo Fsihi ya wakati huu ilienda sambamba kabisa
na mabadiliko ya jamii.
Kipindi cha vita ya kagera,Hiki ni kipindi
a,mbapo jamii ilikuwa katika vita ambapo watu wengi walijawa na hofu kubwa
kutokana na vita hiyo ,ambapo watu walipoteza mali, maisha na kulikuwa na
kuwabeba vijana katika vita ambapo walipigana ili kutetea taifa la Tanzania.Riwaya
ziliandikwa kuhimiza vijana waeze kujikaza na kuwa jasiri katika katika
kupambana na hali hiyo ya vita .Kukaandikwa riwaya kama “Mashujaa
wakaza kamba”(1978) riwaya iliyoandikwa na P.Shija”Vita hivi vya Uganda na
Tanzania viliibua waandishi walioandilka
riwaya zilizolenga kuwatia moyo, na
kuwapa hamasa au kuwahamasisha vijana hao, pia kulenga kusisitiza ukakamavu,wawapo
vitani . Hivyo asihi ya wakati ilisadifu maisha halisia ya kipindi hiki.
Kipindi cha utandawazi, Hiki ni kipindi
ambacho kimetawaliwa na maendeleo ya sayansi na teknolojia, ambapo katika
kipindi hiki kulizuka soko huria, ambapo jamii ya kipindoi hiki ilianza kuishi
kwa kuiga mambo mbalimbali kutoka katika mataifa ya kimagharibi , kukatokea
mambo mengi ambayo yanahusisha kutafuta mali kwa nguvu, kizazi au jamii
iliyojaa na tamaa, umasikini ulliokithiri, umalaya na mitandao ya kijamii
iliyochangia kuharibu maadili ya watu .Katika kipindi hiki kumeibuka dhamira za
riwaya zinazolenga kueleza mambo mazito ya kijamii, kama vile mauaji ya albino,
kutokana na dhana potofu walizonazo watu wa kipindi hiki.Kutokana na ukatili
huo ziliibuka riwaza ya “Takadini” iliyoandikwa na Ben Hanson
,pia kuna masuala ya mapenzi yanayopelekea watu kupoteza kazi,pia mapenzi
yanapunguza ufanisi katika kazi, mfano riwaya ya “Mfadhili” iliyoandikwa na “Hussein Tuwa” (2004), na kitabu
kinachoongelea masuala ya umasikini “Usiku
utakapokwisha” kilichoandikwa na “Mbunda Msokile”(1990) na masuala ya tamaa, ambapo watu wa jamii ya
kipindi hiki wametawaliwa na tamaa zinazowapelekea kuingia katika matatizo
makubwa, mfano riwaya ya “Kiroba cheusi”
kilichoandikwa na “Laura Pettie” (2019), ambaye anwatumia wahusika Morena na
Fatumata kueleza suala la tamaa na matatizo ya tamaa.Hivyo kutokana na
mabadiliko ya jamii riwaya nayo imekuwa ikibadilika vivyo hivyo.
Hivyo basi fasihi na jamii ni vitu viwili
ambavyo ni kama baba na mtoto haviwezi kutenganishwa ,kwa kuwa fasihi
inachipukia kutoka katika jamii na mabadiliko hayo ya kijamii ndio mwongozo au
chanzo cha fasihi mpya.Na jamii sio mgando bali ina mabadilika badilika
kutokana na vipindi tofauti ambavyo vinaikumba jamii hiyo, na fasihi nayo
inafuata mabadiliko hayo
MAREJELEO
Mulokozi
M. M, (2017). Utangulizi wa fasihi ya
Kiswahili;Muccoi Printing Press:Dar-es-salaam
Msokile,
M.(1990). Usiku utakapokwisha.Dar es
salaam University Press: Dar-es-salaam
Kezilahabi,
E. (1999).Kaptula la Marx.Dar es
salaam University Press: Dar-es-salaam
Pettie
L, (2019);Kiroba cheusi;Mfuko wa
riwaya ya waridi:Dar-es-salaam
No comments:
Post a Comment