1. (a).
Tathimini mtihani wa kidato cha nne mwaka 2018.Kisha onesha uhalali na
kuaminika kwake
MPANGO KAZI
UTANGULIZI
·
Maana ya mtihani
·
Maana ya tathmini
KIINI
·
Ubora na udhaifu wa mtihani wa kuhitimu
kidato cha nne (2018).
HITIMISHO
MAREJELEO
Mtihani,ni njia ambayo mtu hupimwa
kutokana na alichokisoma au alichofundishwa ili atambuliwe kwamba alielewa au
hakuelewa. Ni njia rasmi zaidi ya kupima mafanikio katika mchakato wa
kufundisha na kujifunza baada ya kipindi maalaumu kumalizika.Tathimini,ni utaratibu
wa kupima na kuchunguza hali halisi kwa lengo la kupata data zitakazomwezesha
mwalimu au mtahini kufanya maamuzi yanayohusu urekebishaji au uboreshaji wa
mambo mbalimbali katika elimu. Hivyo mchakato wa tathimini huchambua ,hukusanya na kuzipa daraja la ubora taarifa za
ufundishaji na ujifunzaji ili kuamua ni
kwa kiasi gani malengo yaliyoainishwa kwenye mtaala yamefanikiwa. Ifuatayo ni
tathimini ya mtihani wa Taifa wa Kiswahili kidato cha nne (2018).Kwa kuanza na
ubora wake;
Maelezo yaliyotolewa katika kila sehemu
ya mtihani yapo wazi, uwazi wa maelezo unamsaidia mwanafunzi kuyaelewa na
kuyajibu vyema maswali yanavyotakiwa kujibiwa, pia katika maelezo ya jumla ya
mtihani mfano, “sehemu “B” (Alama 25) Sarufi na Utumizi wa lugha”, jibu maswali
yote katika sehemu hii, uwazi huu humsaidia mwanafunzi kujua sehemu husika
inahitaji nini, na mada husika ya maswali hayo.
Maswali yanaendana na kiwango cha elimu
cha watahiniwa, katika mtihani huu wa kidato cha nne (2018 ), maswali yaliyomo
yametolewa kwa kuzingatia mada za
kiwango cha elimu ya Tanzania kwa ngazi ya elimu ya sekondari, pia mada
zimechukuliwa kama muhtasari ulivyo ainisha mada hizo,mfano, maswali ya ufahamu
, insha na maswali ya kutoa ufanano na utofauti wa baadhi ya dhana katika mada.
Uwazi wa maswali ya mtihani, maswali
yaliyotolewa yana maelekezo wazi na yanaonesha kwa uwazi swali lijibiwe kwa
namna ipi , kwani baadhi ya maswali humpa ugumu mwanafunzi, lakini katika
mtihani huu ni bora kwa mwanafunzi wa
kidato husika ambapo humwezesha hata kujibu swali vyema, mfano ; sehemu
“A”(Alama 10), Ufahamu “Soma kwa umakini kifungu cha habari kifuatacho kisha
jibu maswali yanayofuata”. Hii itamrahisishia mwanafunzi kujibu vyema.
Licha
ya ubora huo wa mtihani huu, pia mtihani huu wa kidato cha nne (2018), una
mapungufu yafutayo;
Muda wa kuanza na kumaliza mtihani
haujabainishwa kama inavyotakiwa, kwa mfano katika mtihani wa Taifa wa
Kiswahili kidato cha nne (2018), maelekezo ya muda yana utata kwani katika
mtihani huu imeonyeshwa “muda : saa 3:00”, muda huu haujawa wazi kwani
hawajaonesha mtihani unaanza saa ngapi
na kumalizika saangapi. Na pia
maelezo hayo yana utata kati ya mtihani unaanza saa tatu kamili au unafanyika
kwa masaa matatu.
Katika
mtihani huu sehemu “A” na “B” mgawanyo wa alama haujaoneshwa kulingana na swali
mojamoja isipokuwa alama zimewekwa kwa ujumla katika sehemu hizo, pia katika
maswali ya insha sehemu “C”,”D” na “E” alama zimebainishwa
katika swali lakini katika vipengele vya
swali kwa mfano utangulizi, kiini na
hitimisho hawajaonesha idadi ya alama za vipengele hivyo.
Kutokutolewa kwa idadi ya maneno katika kuandika kichwa
cha ufahamu,Katika mtihani sehemu “A” swali la kwanza kipengele (d) swali linamtaka mwanafunzi kuandika kichwa cha habari kinachofaa
kwa habari aliyoisoma, lakini hawajatoa au kumwelekeza mwanafunzi ni maneno
mangapi anapaswa kuyaandika kwenye kichwa cha habari hicho.
Mtihani haujazingatia utungaji wa aina
mbalimbali za maswali , kwa mfano katika mtihani hakuna maswali ya kuchagua
jibu sahihi, maswali ya kuoanisha, pamoja na maswali ya kuandika kweli au si
kweli, isipokuwa maswali mengi yaliyo katika mtihani yanahitaji maelezo zaidi mfano, maswali
sehemu “C” ambayo ni ya insha pamoja na
maswali ya sehemu “B”.
Kutobainishwa kwa idadi ya hoja zinazohitajika katika baadhi ya maswali, kwa mfano swali la (8) hawajabainisha ni hoja ngapi zinahitajika katika kutofautisha muundo wa barua rasmi na barua za kindugu au kirafiki. Kutokubainisha idadi ya hoja zinazohitajika katika swali husika huweza kupelekea mwanafunzi kuandika hoja nyingi na kusahishiwa hoja baadhi zingine zilizobaki hapewi alama anazostahili au kutokusahishiwa kabisa.
Hivyo
ni muhimu mitihani kutungwa kwa kuzingatia uhalali na uhakika ili kupima
kiwango kilichotarajiwa kwa mwanafunzi kwa kipindi fulani cha muda, kwa mfano
matumizi ya maneno magumu katika mtihani yatamfanya mwanafunzi asing’amue
maswali na hivyo kutojibu ipasavyo na
kupelekea lengo kusudiwa kupotea.
MAREJELEO
Baraza la mitihani Tanzania (2018). Mtihani wa Kiswahili wa kuhitimu kidato cha nne.Dar-es-salaam:Baraza
la mitihani Tanzania
No comments:
Post a Comment