Sunday, February 6, 2022

 

KUSH: DAWA MPYA YA KULEVYA NCHINI SIERRA LEONE





Wakati janga la madawa ya kulevya kama vile  likiendelea katika nchi mbalimbali duniani.

 Nchi ya Sierra Leone imegundua dawa mpya ya haramu inayojulikana kwa jina la Kush ambayo huuzwa kwa bei nafuu, na hivyo kupendwa na watu wengi nchini humo hususani ya vijana. Na inaripotiwa kuwa dawa hii huenda ikawa na ukali zaidi ya dawa za kulevya kama vile heroin na cocein.

Ripoti ya hospitali kutoka mji mkuu wa nchi hiyo Free town inasema kuwa “asilimia tisini (90%) ya wanaume walilazwa katika hospitali hiyo wamekutwa na ugonjwa wa akili kutokana na matumizi ya kush.

Jeshi la polisi katika nchi hiyo imejiandaa vikali juu ya matumizi na usambazaji wa dawa hizo haramu.

Chanzo: BBC


No comments:

Featured Post

 SOMA SIMULIZI ZENYE KUSISIMUA HAPA A. UTAJIRI WENYE UCHUNGU     UTAJIRI WENYE UCHUNGU-1     UTAJIRI WENYE UCHUNGU-2      UTAJIRI WENYE UCH...