UTAJIRI WENYE UCHUNGU - 3

Sehemu Ya Tatu (3)


“Usijali, na mama naye anaendeleaje?”

“Anaendelea vizuri tu, anaendelea kutibiwa, asante sana kwa msaada wako...”

“Usijali! Nipo kwa ajili ya kukusaidia kama rafiki yangu...” alisema Dylan.

Walikuwa wakiongea maneno mengi, wakati Dylan akifikiria kwamba msichana huyo alikuwa rafiki yake wa kawaida tu, kwa Pauline hali ilikuwa tofauti kabisa, kwake alimuona mwanaume huyo kuwa mpenzi wake, hivyo hata alipoambiwa kwamba yeye alikuwa rafiki tu, moyo wake ulimuuma mno.

****

Hakukuwa na msichana aliyekuwa akimfikiria kichwani mwake kama alivyokuwa Katty, huyo alikuwa msichana pekee ambaye kwa kipindi hicho alitamani sana kumuona.

Mwaka wa pili ulikuwa umekatika lakini hakuweza kukutana na msichana huyo. Katika kipindi ambacho alikuwa Qatar, aliwasiliana naye na kumwambia kwamba anataka kuonana naye kwa mara nyingine.

Kwa kuwa Katty alimwambia kuwa katika kipindi hicho alikuwa mjini Dubai, hivyo akamuahidi kwamba ilikuwa ni lazima amfuate na kuonana naye kwani kutoka Dubai mpaka Qatar hapakuwa mbali, ilikuwa ni kama kilometa elfu moja tu kwani zote hizo zilikuwa katika muunganiko wa nchi za Kiarabu, Emirates.

“Unataka nije lini?” aliuliza Katty.

“Siku yoyote, ukishindwa, hata mimi naweza kuja.”

“Sawa! Naomba tufanye kesho, nitakuja mara moja kisha nitarudi...”

“Hakuna tatizo!”

Moyo wake ulikuwa kwenye presha kubwa, tangu aanze ukaribu na msichana huyo hakuwa ameonana naye tena kitu kilichomuumiza na kumpa mawazo mno. Miaka miwili ilikuwa mingi sana kwake, hakutaka kuvumilia, hakutaka kuona mwaka huo unakatika pasipo kuonana naye.

Kitendo cha kuambiwa kwamba kesho angeonana na Katty kilimpagawisha mno, hakuamini, akajiandaa vilivyo ila tatizo lililokuja lilikuwa ni afya yake tu.

Hicho ndicho kilichomtia uchungu, alikuwa tajiri, lakini kuwa tajiri pasipo jogoo wake kuwika, utajiri ukawa mchungu mno kwake. Kitu alichokuwa akikifikiria kipindi hicho ni namna gani angeweza kulala na msichana huyo pasipo kugundua kama kiungo chake hakikuwa kikifanya kazi.

Alichokifanya ni kuondoka na kuelekea katika duka linalouza dawa za kuongeza nguvu na hata midoli ya kufanyia mapenzi. Aliingia ndani ya duka hilo kisiri, hakutaka mtu yeyote yule afahamu, alivalia kofia kubwa na miwani.

Alipoingia, akanunua kifaa alichokihitaji na kisha kuondoka zake huku akimsubiri msichana Katty afike Qatar na kuzungumza naye, ikiwezekana usiku mzima walale wote.

Ilipofika saa moja usiku, akapigiwa simu na Katty na kuambiwa kwamba tayari msichana huyo alikwishafika katika uwanja wa ndege hivyo amuelekeze hoteli aliyofikia amfuate.

Ndani ya dakika kadhaa, msichana Katty alikuwa mapokezi. Dylan alipopigiwa simu na kuambiwa kwamba kulikuwa na mgeni wake, hakutaka kumwambia dada wa mapokezi amruhusu aende huko bali alitoka na kuelekea chini, alitaka kumpokea yeye mwenyewe.

Alipofika, kitu cha kwanza baada ya kumuona ni kumkimbilia na kumkumbatia huku kila mmoja akionekana kuwa na furaha kubwa. Watu waliokuwa mahali hapo, wakabaki wakiwashangaa tu, mapokeo waliyopokeana watu hao ilikuwa tofauti kabisa na watu wengine.

Hawakutaka kubaki mahali hapo, walichokifanya ni kuifuata lifti huku wakiwa wameshikana kimahaba, walipoingia ndani, wakaanza kupanda juu huku wakishikana hapa na pale.

“Ninakuhitaji usiku wa leo,” alisema Katty, yeye mwenyewe hakufikiria kama siku hiyo angekuwa namna hiyo kwani hata kuzungumza na Dylan kwa kipindi kirefu tangu afike, hawakuzungumza.

“Nitafanya lolote utakalo, mpaka utaridhika...”

“Kweli?”

“Niamini mpenzi!”

Walipofika katika floo waliyokuwa wakienda, wakateremka, wakashikana kimahaba mpaka ndani ya chumba walichochukua, kuingia ndani, hawakutaka hata kuzungumza chochote kile, wakaelekea kitandani.

“Naomba...naomba, nataka unipe,” alisema Katty huku akilalamika kimahaba.

“Nakupa, nakupa mpenzi...”

Wakati Dylan akisema maneno hayo, hakukuwa na mabadiliko yoyote yale mwilini mwake, alikuwa kama mtu aliyekuwa akila chakula huku akiwa na mawazo tele.

Wakati Katty akiendelea na utundu wake mwilini mwake ndipo akakumbuka kwamba alikuwa na kifaa chake katika droo na ilikuwa ni lazima kitumike usiku huo.

Akili yake ilicheza kwa haraka sana, akasimama na kuifuata taa, akaizima na kurudi kitandani. Katty alikuwa hoi, hakujiweza, alichokuwa akisubiri ni kuanza kwa mechi tu.

Kwa siri sana akaupeleka mkono wake kwenye droo ya kitanda na kutoa kifaa alichotakiwa kukitumia na kujiweka tayari, macho yakawa yakimwangalia Katty ambaye alifumba macho kwa hisia kali.

“Upo tayari?” aliuliza huku akiwa amevaa, tena kwa kufunga kamba kiunoni.

“N..ip..o tay..ar..i...” alijibu Katty huku akitoa pumzi nzito kimahaba.

Kilichofuatia baada ya hapo ni miguno ya mahaba kutoka kwa wote wawili, kitanda kililia sana, kila mmoja alikuwa akihema kwa nguvu, Katty, kwa jinsi alivyokuwa na hamu na Dylan, muda wote alikuwa akimvuta kwake, alimng’ang’ania sana huku aking’atang’ata sikio na shingo ya Dylan.

****

Baada ya dakika kadhaa, kila mmoja alikuwa hoi, kwa haraka sana hata kabla Katty hajagundua, Dylan akasimama na kuelekea chooni. Katty hakushtukia kitu chochote kile, kwa kuwa kulikuwa na giza hata kumuona vizuri hakumuona, ndiyo kwanza akageukia upande wa pili na kulala.

Kule chooni, Dylan akakitoa kile kiungo cha bandia, akakisafisha na kisha kuanza kurudi nacho chumbani ambapo akafungua droo ya kitanda na kukihifadhi, tena kwa kukifichaficha chini ya makaratasi na yeye kulala.

Asubuhi ya siku iliyofuata, wote wakaamka, wakanywa chai, wakatoka mahali hapo na kuelekea katika bwawa la kuogelea ambapo waliogelea mpaka mida ya saa tano wakatoka na kwenda kunywa chai.

Katika kipindi chote hicho, wote wawili walionekana kuwa na furaha tele, kila mmoja hakuamini kama mwisho wa siku wangekuwa hivyo wawili. Walipiga stori, walipomaliza wakaelekea chumbani ambapo muda wote Katty alikuwa akililia kurudiwa kwa mchezo.

“Nataka tena....” alisema Katty huku akianza kumvua nguo Dylan.

“Subiri kwanza....”

“Nina kiu mpenzi, nimekumisi, nimeyamisi mambo yako,” alisema msichana huyo huku akimbembeleza.

Japokuwa alimuonea huruma msichana huyo lakini hakuwa na jinsi, asingeweza kumsaidia kwa sababu haikuwa usiku na kama angefanya naye ilikuwa ni lazima msichana huyo agundue kwamba kiungo kilichokuwa kikitumika hakikuwa halisi bali kilikuwa bandia.

Alishikwa hapa na pale, alinyonywa huku na kule lakini mwili wake haukubadilika hata kidogo, ulikuwa vilevile pasipo mabadiliko yoyote yale. Katty hakuacha, aliamini kwamba angeweza kumbadilisha mwanaume huyo na kumpa ashki ya kufanya mapenzi lakini pamoja na jitihada zote hizo, majibu yalikuwa bila-bila.

“Kwa hiyo hutaki?” aliuliza Katty huku macho yake yakianza kuwa mekundu.

“Mpenzi! Ninasikia uchovu, nahisi naumwa...”

“Tatizo nini?”

“Sijajua, ila naumwa, sijisikii vizuri...”

Katty alikasirika, mwili wake uliwaka moto, hakutaka kusikia kitu chochote kile, alichokuwa akikitaka ni kufanya mapenzi na mpenzi wake mpya, kuambiwa kwamba hakuwa akijisikia vizuri, roho yake ilimuuma mno. Hakuendelea kumshikashika tena, alichokifanya ni kujilaza pembeni na kutulia zake.

Dylan alikaa siku kadhaa huko Dubai, akaagana na mpenzi wake ambaye alirudi Qatar na yeye Marekani. Njiani, kila mmoja alikuwa na majonzi tele, walizoeana sana, Katty alimpenda mno Dylan, kwake, alikuwa mwanaume mwenye ndoto naye ambaye alijitolea maisha yake kwa ajili yake.

Hata kwa Dylan, hakukuwa na msichana ambaye alikuwa na mapenzi ya dhati kama aliyokuwa nayo kwa Katty. Walitumiana picha huku wakiwa kwenye mapozi mbalimbali, waliwasiliana wakiwa njiani huku ishara nyingi za kimapenzi zikionekana kati yao.

Alipofika nchini Marekani, miongoni mwa watu waliofika mahali hapo kwa ajili ya kumpokea alikuwa msichana Pauline. Dylan alishangaa, hakutaka msichana huyo afike hapo, taarifa aliipa familia yake na watu wengine wa karibu, cha kushangaza, msichana huyo naye alifika kwa ajili ya kumpokea.

“Nimekukumbuka sana Dylan...” alisema msichana Pauline wakati alipokuwa akimkumbatia.

“Nimekukumbuka pia...”

Hakumkumbuka Pauline hata kidogo lakini kwa kuwa aliambiwa hivyo, akaona si tatizo kama naye atamwambia hivyohivyo. Wakaondoka hapo uwanja wa ndege na kuelekea nyumbani, muda wote huo msichana huyo alikuwa karibu naye mno kitu kilichowapa maswali mengi ndugu zake, hasa Catherine.

“Huyu ndiye yule msichana uliyeniambia?” aliuliza Catherine.

“Yupi?”

“Yule Katty!”

“Hapana!”

“Na huyu naye nani?”

“Ni mfanyakazi wangu!”

“Mfanyakazi wako au mpenzi wako?”

“Mfanyakazi!”

“Sasa mbona yupo hivyo, yaani beneti kana kwamba mpenzi wako?”

“Hata mimi mwenyewe nashangaa...” alijibu Dylan.

Muda huo walikuwa nyumbani, walitulia huku wakila na kunywa, ukaribu ule bado uliendelea kuwatia maswali wengine lakini Dylan hakutaka kujali kwani tayari alihisi kwamba kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea moyoni mwa Pauline.

Alikuwa msichana mrembo mno, hata naye moyo wake alihisi kama kulikuwa na kitu kilianza kuingia ila hakutaka kujiweka kirahisi, hakutaka kuona akimsaliti msichana Katty kwa sababu ya Pauline.

Siku hiyo walikaa nyumbani hapo mpaka usiku, tena kwa Dylan kumng’ang’aniza kuondoka kwani bila kufanya hivyo, tayari Pauline alitaka alale nyumbani hapo.

“Naomba nikueleze kitu Dylan...” alisema Pauline huku wakiwa njiani kuelekea nyumbani.

“Kitu gani?”

“Unahisi nini kuhusu mimi?” aliuliza.

“Sihisi chochote...kuna nini kwani?” aliuliza Dylan, wakati huo alikuwa akiendesha gari.

“Haujahisi kwamba nakupenda?”

“Kunipenda?”

“Ndiyo! Ninakupenda, nimekuwa nikitamani kukwambia hili kwa kipindi kirefu sana...” alisema msichana huyo.

“Kunipenda mimi?”

“Ndiyo!”

“Mbona umechelewa sana?”

“Nimechelewa? Hapana! Sijachelewa, nimekuwa nikikufuatilia kwa kipindi kirefu, ukiniambia kwamba una mpenzi, sitokubaliana nawe,” alisema msichana huyo kwa sauti ya upole.

“Nina mpenzi Pauline, na hata nilipokwenda Dubai, nilionana naye, anaitwa Katty!” alisema Dylan.

Kwa Pauline, hakutaka kukubali hata kidogo, alimfahamu Dylan, tangu awe naye, hakukuwa hata na siku moja ambayo alimuona mwanaume huyo akiwa na msichana. Si kumuona tu hata kusikia tetesi kwamba alikuwa na mwanamke yeyote, hakuwahi kusikia.

Kitendo cha Dylan kumwambia kwamba alikuwa na msichana, kilimuumiza na kuona kwamba mwanaume huyo hakutaka tu kuwa naye. Hiyo ilimuumiza mno, alikosa furaha, akajikuta macho yakianza kuwa mekundu na hapohapo machozi kuanza kumtoka.

“Dylan...unanidanganya...kwa nini hutaki kuniambia ukweli?” aliuliza Pauline huku akilia.

“Ndiyo ukweli huo?”

“Unanidanganya, huo ni uongo...unaniumiza Dylan...” alisema msichana huyo huku sauti ya kilio chake ikizidi kuwa kubwa.

“Ndiy...” alisema Dylan lakini hata kabla hajamaliza sentensi yake, tena huku gari likiwa kwenye mwendokasi wa 80, hapohapo msichana huyo akaufungua mlango, kilichotokea, akajirusha barabarani. Dylan macho yakamtoka.

****

Dylan akafunga breki, hakuamini kilichotokea, alichanganyikiwa, harakaharaka akateremka kutoka garini mwake na kuelekea kule msichana Pauline alipojirusha.

Kitu ambacho alimshukuru sana Mungu ni kwamba nyuma hakukuwa na gari lolote lile. Pauline alikuwa amebimbirika mpaka pembeni ya barabara, Dylan alipomfikia na kumwangalia, alikuwa amechubuka mno, mikononi, miguuni na hata mgongoni.

Moyo wa Dylan uliumia mno, hakutaka kuchelewa, hapohapo akambeba na kuanza kuondoka naye huku hata yeye mwenyewe machozi yakianza kumtoka kwani hakuamini kama msichana huyo angefanya hivyo.

“Pauline! What have you done?” (Umefanya nini Pauline?) alimuuliza huku akiwa mikononi mwake.

Alipomfikisha garini, hakutaka kubaki mahali hapo, akaondoka na breki yake ya kwanza ilikuwa ni kwenye Hospitali ya St. Angel Medical Center iliyokuwa hapohapo New York.

Kitendo cha kufika hapo huku akiwaita manesi, tayari machela ikafikishwa, akaufungua mlango na kumtoa msichana huyo. Manesi walipomuona Pauline, hawakuamini, msichana yule alichubuka sana, kabla ya kuuliza chochote kile, wakaisukuma machela ile kuelekea ndani ya jengo la hospitali hiyo.

Walipofika katika chumba kilichoandikwa theatre kwa nje, akaambiwa asubiri kwani humo ndipo ambapo msichana huyo alitakiwa kufanyiwa matibabu kutokana na hali yake kuwa mbaya namna ile.

Dylan alibaki nje, bado alikuwa haamini kilichotokea, kwake, aliendelea kumshangaa msichana huyo, alionekana kuwa mtu wa ajabu na hakufikiria kabisa kama msichana huyo angeweza kufanya jambo hilo.

Akampigia simu Catherine na kumwambia kile kilichotokea. Hakutaka kumwambia mtu yeyote yule kwani msichana huyo, mbali na undugu waliokuwa nao, walikuwa marafiki wa karibu mno.

“Yaani amejirusha kutoka garini?” alisikika Catherine akiuliza.

“Ndiyo!”

“Ilikuwaje?”

“Yaani wewe acha tu...”

“Wewe niambie ilikuwaje!”

“Njoo kwanza..”

“Nakuja!”

Dylan hakutaka kumwambia katika simu, alitaka kuonana naye na kumwambia kile kilichotokea. Baada ya dakika kadhaa, msichana huyo akafika hospitalini hapo na moja kwa moja kuanza kuzungumza naye.

“Kwa hiyo unamaanisha alivyokutaka, ukamkataa?” aliuliza msichana huyo.

“Nilimwambia kwamba nina mtu...”

“Na kweli unaye?”

“Ndiyo!”

“Mbona hukuniambia?”

“Ndiyo nilitaka kukwambia, ni yule Katty ambaye nilionana naye Dubai,” alijibu Dylan.

“Kwa hiyo itakuwaje kwa huyu msichana?”

“Yaani hapa nimechanganyikiwa! Anaweza kujiua huyu!” alisema Dylan.

Waliendelea kusubiri hospitalini hapo mpaka pale ambapo madaktari walipomaliza na kuwataka kumjulia hali mgonjwa wao. Wakaingia ndani ya chumba kile, Pauline alikuwa kimya kitandani, bandeji zilifungwa katika sehemu kubwa ya mwili wake.

Dylan alipomwangalia msichana huyo, moyo wake ulimuuma mno, alimuona jasiri ambaye alikuwa tayari kufanya lolote kwa ajili ya moyo wake. Japokuwa msichana huyo alikuwa na mapenzi ya dhati kwake lakini Dylan hakutaka kujihusisha naye kabisa.

“Ila ni msichana mrembo sana Dylan...” alisema Catherine.

“Nakubaliana na wewe...ila nina msichana tayari...”

“Kwa hiyo itakuwaje kuhusu huyu?”

“Sijajua kwani hata ndoto za kumuacha Katty, sina...”

Wakati wakizungumza hayo, Pauline alikuwa kimya kitandani pale. Alibaki kwenye hali hiyo kwa saa moja, akayafumbua macho yake, watu wa kwanza kukutana nao walikuwa ni Dylan na Catherine.

“Dylan....” aliita msichana huyo kwa sauti ya chini.

“Nipo hapa...” alijibu Dylan huku akimsogelea msichana huyo.

“Niambie kitu kimoja....”

“Kitu gani?”

“Unanipenda?” aliuliza msichana huyo akimwangalia Dylan usoni, Catherine alikuwa pembeni akiangalia kinachoendelea.

“Sikiliza Pauline....ni laz...”

“Niambie moja, unanipenda?” aliuliza msichana huyo.

Jibu ni kwamba hakumpenda, hakuhisi hisia zozote za mapenzi moyoni mwake lakini kumwambia ukweli kwamba hakuwa akimpenda, alihisi kungeibua tatizo jingine kabisa.

Alibaki akimwangalia msichana huyo, hata kama angesema anampenda, ingekuwa ni kumwambia kwa sababu tu hakutaka apate tatizo lolote lile. Pauline aliendelea kumwangalia Dylan, kitu alichotaka kusikia ni jibu kutoka kwa mwanaume huyo.

“Ninakupenda....” alisema Dylan, hata kuongea kwake ilikuwa ni kujilazimisha tu.

“Una uhakika?”

“Ndiyo! Ninakupenda Pauline...” alisema Dylan.

Msichana huyo akatoa tabasamu pana, hakuamini alichokisikia. Kwa kipindi kirefu alitaka kusikia mwanaume huyo akimwambia anampenda hivyo kuambiwa hivyo, kwake ilikuwa faraja tele.

Akajitahidi kuinuka kitandani pale na kisha kumkumbatia Dylan. Muda wote huyo, Catherine alibaki akiwaangalia tu. Msichana aliyekuwa mbele yake, hata kwa kumwangalia tu, alionekana kuwa na mapenzi ya dhati kwa kaka yake.

“Nataka unioe...” alisema Pauline kwa sauti ya chini kabisa, karibu na sikio la Dylan.

“Nikuoe?”

“Ndiyo!” alijibu msichana huyo.

“Lakini Pauline!”

“Nakuomba Dylan...ninakupenda sana...” alisema msichana huyo.

Hata kabla Dylan hajatoa jibu lolote kuhusu suala la Pauline kutaka kuolewa, hapohapo akasikia simu yake ikianza kuita. Harakaharaka akaitoa kutoka mfukoni mwake, hisia zake zilimwambia kwamba mpigaji alikuwa baba yake tu ambaye angemuuliza mahali alipokuwa.

Pauline alifuatilia, naye mwenyewe alitaka kumfahamu mpigaji. Dylan alipoitoa simu ile na kuangalia kioo, jina la Katty lilionekana vizuri, moyo wake ukapiga paaa......Pauline akanyong’onyea, akajikuta akianza kuishiwa nguvu.


‘Dylan Was Caught With Beautiful Shawty’ ‘Alone In The Dark, What Did They Do?’ ‘Atlast, He Is Happy Maybe’ (Dylan Abambwa na Msichana Mrembo’ Ni Gizani, Walikuwa Wakifanya Nini?’ Hatimaye! Labda Ana Furaha) hivyo vilikuwa vichwa mbalimbali vya magazeti ya udaku, kila mtu aliyeyaona mitaani, tena yakiwa na habari iliyomhusu mtoto wa bilionea, iliwashangaza na hivyo kulinunua gazeti hilo.

Dylan alionekana kuwa na msichana mrembo, mwenye mchanganyiko wa rangi, walipomwangalia msichana huyo, alikuwa mrembo wa sura kiasi kwamba kila mmoja alishangaa, jamaa alimtoa wapi msichana huyo?

Hiyo ilikuwa habari kubwa ya siku hiyo, ukaribu wao, ulionyesha shaka kwa kila mtu aliyeziangalia picha zile, walichokifanya wataalamu wa mambo, wakachukua magazeti yenye picha hizo kisha kuanza kuzitolea ufafanuzi.

Kitu cha kwanza walichoanza nacho kilikuwa ni muonekano wa wote wawili, walisimama karibukaribu, mbali na hiyo, walionekana kama watu wenye uhusiano wa kimapenzi kitu kilichozua maswali kwani walijua kwamba huyo Dylan alitarajiwa kumuoa msichana mwingine siku chache zijazo.

“Au huyu ndiye msichana mwenyewe?” aliuliza jamaa mmoja.

“Sidhani! Nasikia huyo ni mrembo zaidi, anaitwa Katty, huyu ni Pauline, ndiye nani? Si huyu,” alisema jamaa mwingine, alionekana kumfuatilia sana Dylan.

Taarifa hizo ilipomfikia Dylan, alishangaa, hakuamini kama kitendo chake cha kusimama na msichana Pauline kingekuwa stori namna ile, alijifungia ofisini mwake, hakutaka kutoka ndani na kitu pekee kilichomuumiza ni juu ya Katty, kama angeona kile kilichoandikwa, nini kingetokea?

Wakati hayo yakiendelea, katty alikuwa nchini Italia, alikwenda huko tayari kwa kuonana na padri ambaye alitakiwa kufungisha ndoa yao miezi miwili mbele. Wakati wakiwa mitaani ndipo macho yao yakatua katika Gazeti la US Weekly ambalo hutoka kila siku na kusambazwa katika nchi zenye maendeleo, alipoliona, akamwambia rafiki yake alichukue kwani habari iliyoandikwa, ilimshtua.

Alipopewa mikononi na kuliangalia, hakuamini kile alichokiona, damu ikaanza kutembea kwa kasi mwilini mwake, hakuamini kama mwanaume aliyekuwa akimpenda, Dylan angeweza kuwa katika hali hiyo, tena na mwanamke ambaye hakuonekana kuwa mrembo kama yeye.

“Cassie, am I dreaming?” (Cassie, ninaota?) alimuuliza rafiki yake.

Hakuweza kuyazuia machozi yake kutiririka mashavuni mwake, maumivu aliyoyasikia hayakuweza kusimulika. Hata nguvu za kwenda kumuona Padri hakuwa nazo, alibaki akisononeka moyoni mwake tu.

“Katty, usijali, inawezekana ni marafiki tu...” alisema Cassie.

“Marafiki! Marafiki wanaweza kusimama hivi?” aliuliza Katty.

“Ni kawaida tu, usimfikirie vibaya Dylan, ni wako na bado anakupenda.”

Japokuwa rafiki yake, Cassie alimwambia hivyo lakini hakutaka kuamini, bado alihisi kwamba mpenzi wake huyo alikuwa akimsaliti. Hakutaka kumpigia simu kwanza mpaka pale atakapozungumza naye kwenye simu ili ajue kuhusu kile kilichokuwa kimetokea.

Wakati akiwa na padri huyo huku wakizungumza, simu yake ikaanza kuita, alipoangalia mpigaji, alikuwa mpenzi wake, Dylan. Hakuipokea simu hiyo, alibaki akiiangalia, alitaka kuzungumza na mwanaume huyo pale atakapotoka nje.

Walipomaliza kuzungumza na padri huyo, wakasimama na kutoka huku wakiwa wamekwishaelewana kwamba yeye ndiye atakayefungisha ndoa hiyo ambayo ilionekana kuwa na dalili zote za kufana.

“Dylan alinipigia simu...” alisema Katty.

“Amesemaje?”

“Nilikuwa ndani, sikuweza kupokea...”

“Hebu mpigie kwanza,” alisema Cassie, hata kabla Katty hajapiga, mara simu ya Dylan ikawa inaingia, harakaharaka akaipokea.

“Unasemaje?” aliuliza kishari.

“Samahani, naomba nikuelezee...” alisema Dylan.

“Unielezee kuhusu nini? Kuhusu nini nauliza? Au huyo malaya wako?” aliuliza Katty huku hata sauti yake tu ilisikika kama mtu mwenye hasira nyingi.

“Hapana! Usiseme hivyo!”

“Nisemeje? Nakuuliza swali, unamjua yule mwanamke humjui?” aliuliza msichana huyo.

“Namjua!”

“Ni nani kwako?”

“Mfanyakazi wangu!”

“Kwa hiyo umeamua kuanza kuchukua wafanyakazi?” aliuliza msichana huyo.

Ilikuwa ngumu kumtuliza, lakini kwa sababu Dylan alikuwa mtu mwenye busara, nguvu ya kuzungumza na watu, akamuweza Katty na kuanza kumhadithia kila kitu kuhusu msichana Pauline.

Hakutaka kumficha kitu chochote kile kwa kuamini kwamba ukweli ndiyo utakaomfanya kuwa huru. Katty akaridhika, historia fupi kuhusu msichana huyo ambayo alipewa, ikampa uhakika kwamba mpenzi wake huyo hakuwa na uhusiano na msichana huyo.

“Una uhakika?”

“Ndiyo mpenzi! Usiamini magazeti, ukienda hotelini kuonana na mgeni, watasema umekwenda kulala na mwanamke, usiyaamini haya magazeti,” alisema Dylan.

Kidogo moyo wa Katty ukawa na amani, akahisi furaha ikirudi tena moyoni mwake, kile alichozungumza mpenzi wake kilimpa uhakika kwamba kweli Pauline hakuwa wa mpenzi wake bali walikuwa watu wasiokuwa na uhusiano wowote ule japokuwa msichana huyo alikuwa akijikomba.

“Umefikia wapi?” aliuliza Dylan.

“Nimezungumza na padri, kila kitu kipo tayari!”

“Kweli?”

“Ndiyo! Kazi imebaki kwetu tu,” alisema Katty.

“Basi hakuna tatizo, kila kitu kitafanikiwa.”

Siku ziliendelea kwenda mbele, kila mtu akawa na hamu kuona harusi hiyo, magazeti yaliripoti kila kitu kilichokuwa kikiendelea. Kwa Dylan, hakuwa na furaha kabisa, kila siku, alikuwa akifikiria kuhusu tatizo la kiafya lililokuwa likimsibu.

Hiyo ilikuwa siri kubwa, hakutaka kumwambia mtu yeyote yule, ni watu watatu tu ndiyo waliokuwa wakilifahamu tatizo hilo, yeye, baba yake na mama yake mlezi.

Moyo wake ulimuuma sana lakini hakuwa na jinsi, siku zilikatika mpaka siku hiyo ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu. Kila kitu kiliandaliwa na ni tukio hilo ndilo lililokuwa likisubiriwa.

Ilikuwa harusi kubwa, iliyoshika masikio ya watu lakini hakukuwa na watu zaidi ya ishirini waliohuhuria, ilikuwa harusi ya kitajiri, na hata hao watu wachache waliotakiwa kuhudhuria, walihudhuria kwa mwaliko maalumu.

“Umekubali kumuoa na kuwa mke wako katika shida na raha?” aliuliza padri.

“Ndiyo nimekubali!”

Hakuishia hapo, padri aliendelea kuuliza na jibu lilikuwa lilelile na hata alipokuja kwa Dylan naye, jibu halikubadilika, liliendelea kuwa vilevile. Makofi yakatawala, siku hiyo usiku, kilichofuatia ni sherehe kubwa na kuelekea katika Visiwa vya Bahamas kwa ajili ya fungate.

Kama kawaida, Dylan alipokwenda huko, kwenye begi lake kulikuwa na kiungo cha bandia ambacho ndicho angekitumia huko. Hilo, bado Katty hakujua chochote kile, kila alipofanya naye mapenzi, hakujua kama kilichokuwa kikitumika kilikuwa ni kiungo cha bandia kutokana na ulaini wa kifaa hicho.

*****

“Unaitwa nani?”

“Mike Johnson...”

“Una miaka mingapi?”

“Ishirini!”

“Sawa! Unaishi wapi hapa New York?”

“Livingstone...”

“Kule uswahilini?”

“Ndiyo!”

“Utaweza kutunza siri...”

“Hakuna tatizo...nitaweza tu....”

“Sawa! Unajua kwa nini upo hapa?”

“Hapana! Ila niliitwa na watu fulani, wakaniambia kuna kazi natakiwa kufanya na nitalipwa dola milioni moja, hakuna tatizo, mimi ni masikini na ninahitaji sana hizo hela, hivyo nipo tayari!”

“Yaani kisa umasikini, haijalishi ni kazi gani, wewe upo tayari?”

“Ndiyo daktari...”

Alikuwa miongoni mwa vijana masikini mno waliokuwa wakiishi katika Mtaa wa Livingstone hapo New York. Maisha yake yalitawaliwa na ufukara mkubwa, hakuwa na fedha, mara nyingi alifanya kazi mbalimbali ili kujikimu na maisha lakini hayakuwa na ahueni hata siku moja.

Umasikini ulimpiga, ulimtesa mno na hakuwa na tumaini lolote lile mbele yake. Alitamani kuwa na fedha, alitamani kuendesha magari ya kifahari na kuishi maisha ya gharama kama walivyokuwa wakiishi masupastaa wa mpira wa kikapu, wanamuziki lakini hilo halikuwezekana, maisha hayo alikutana nayo kwenye ndoto tu.

Japokuwa alikuwa masikini, huyu Mike alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa na sura nzuri, alimvutia kila msichana aliyekuwa akimwangalia, wengi walitamani kuwa naye lakini Mike mwenyewe, yeye na wanawake ilikuwa ni kama paka na panya.

Aliamini kwamba unapojiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi unapoteza asilimia kadhaa ya vitu fulani katika maisha yako, utakuwa na stress, utashindwa kufanya mambo mengine mara mpenzi anapokuzingua hivyo, kuwa singo kama alivyoamua, kwake ilikuwa ndiyo njia sahihi ya kuweza kuishi maisha ya furaha.

“Do you know my father?” (unamfahamu baba yangu) aliuliza msichana mmoja, mzuri wa sura, alisimama mbele ya Mike.

“No! Who is he?” (hapana! Ni nani?)

“Mr. Godfrey Paul...” (Bwana Godfrey Paul)

“A bilionaire one?” (huyu bilionea?)

“Exactly.” (Sawasawa)

“So what can I help you miss?” (Kwa hiyo nikusaidie nini mrembo?)

“I need your help! I have fallen, I want you to pick me up,” (Ninahitaji msaada wako! Nimeanguka, nataka uniinue) alisema msichana huyo.

“How?” (Kivipi?)

“I love you, I want you to be mine, forever!” (Ninakupenda! Nataka uwe wangu, milele) alisema msichana huyo aliyeitwa Jesca.

Japokuwa msichana huyo alijitambulisha kama mtoto wa bilionea mkubwa nchini Marekani lakini Mike hakutaka kukubaliana naye, hakuhitaji msichana yeyote kwa kipindi hicho, hakuwa tayari kwa kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi.

Aliachana na Jesca na yeye kufanya mambo mengine. Umasikini uliendelea kumtesa kila siku, kwa kuwa alikuwa mrefu, aliamini kwamba mchezo wa kikapu ungemtoa lakini napo huko akaambulia patupu.

Maisha yalisonga mbele mpaka siku ambayo alifuatwa na watu wawili, waliovalia suti ambao walimvuta pembeni na kuanza kuzungumza naye. Mara ya kwanza alihisi kuwa hao ni watu wabaya, aliogopa lakini hakutaka kuuonyesha uoga wake mbele ya watu hao.

Walijitambulisha kwamba wao ni watu wema hivyo walitaka kufanya naye kazi. Hakujua ni kazi gani, hakuwa na fedha, alikuwa kijana masikini, je hiyo kazi ambayo alitakiwa kufanya na watu hao, ilikuwa kazi gani?

“Mfanye kazi na mimi?”

“Ndiyo!”

“Sasa mimi nina mtaji gani jamani?”

“Wala usijali, si kazi inayohitaji wewe kutupa fedha, ni kazi inayohitaji sisi kukupa fedha!” alijibu jamaa mmoja.

“Mmh!”

“Usiogope, jiandae, kesho saa mbili asubuhi tunakuja kukuchukua, kuna sehemu tutakwenda nawe. Kwanza chukua hii,” alisema mwanaume mmoja, hapohapo akamgawia kiasi cha dola mia tano, wakaondoka zao.

Huo haukuwa mwisho, bado alikuwa akijiuliza kuhusu watu hao lakini hakupata jibu kabisa. Wakati mwingine alihisi kwamba watu hao walikuwa wauza madawa ya kulevya, akaogopa lakini kwa kuwa walionekana kuwa watu safi, wamevaa suti hakutaka kujali sana wala kuhisi hivyo.

Maisha yakaendelea, kesho yake, muda uleule alioambiwa, watu hao wakafika mahali hapo, wakamchukua na kuondoka naye. Baada ya dakika kadhaa, gari hilo likasimama mbele ya Hospitali ya Marie Stoppes Medical Center na kutakiwa kuteremka, akafanya hivyo.

Wakaelekea ambapo huko akapelekwa kwa daktari mmoja ambaye alimchukua na kumuingiza ndani, kisha akaanza kuzungumza naye, mazungumzo marefu yaliyojaa maswali mengi.

“Kitu cha msingi ni kutunza siri, halafu baada ya kufanya kazi yetu, tunataka hata mji huu uhame,” alisema Dk. Fabian.

“Hakuna tatizo, nitatunza siri mpaka kifo changu!”

“Kweli?”

“Ndiyo! Nitatunza siri dokta!”

“Sawa! Unasema unaishi Livingstone, si ndiyo?”

“Ndiyo dokta!”

“Basi sawa...subiri hapo!”

Mike hakutakiwa kuwa na presha yoyote ile, alitakiwa kukaa kwenye benchi, baada ya muda fulani, wanaume wengine wakaja na kumchukua, wakampeleka katika chumba kimoja kilichokuwa kimya kabisa.

Muda wote huo Mike alikuwa akishangaa, hakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea. Kwa mbali, akaanza kuingiwa na hofu, wakati mwingine alitamani kuwaambia kwamba basi hiyo kazi hakuitaka tena lakini akapiga moyo konde na hivyo kusikilizia nini ambacho kingetokea.

Baada ya saa moja, mlango ukafunguliwa, dokta Fabian akaingia akiwa na vipimo. Kitu cha kwanza kabisa akachukua damu yake na kuondoka nayo, aliporudi, alikuwa na majibu kwamba damu yake ilikuwa safi hivyo alistahili kuifanya kazi hiyo.

“Ila ni kazi gani?”

“Usijali Mike, utaijua tu. Si kazi ya hatari kabisa...si unataka fedha lakini?”

“Ndiyo!”

“Basi usijali...” alisema daktari huyo. Bado Mike alikuwa na hofu mno. Kuna kipindi alifikiria kukimbia tu kwani kila alipokuwa hapo, mapigo yake ya moyo yalikuwa yakidunda kwa nguvu mno.


Kila mmoja alionekana mwenye furaha kubwa huko Bahamas, walitembea kila sehemu, kwa siku zote walizokuwa huko, Dylan alikuwa akifanya mapenzi na mkewe, Katty usiku tu.

Hakutaka kufanya mchana, alijifanya kuwa bize mchana na hata alipoguswa hapa na pale, alikuwa mkali, ila usiku, tena huku taa zikiwa zimezimwa, alifanya kwa nguvu zote kwa kutumia kiungo cha bandia ambacho alikifunga kama mkanda fulani hivi.

Baada ya kukaa kwa mwezi mzima ndani ya kisiwa hicho huku wakiponda raha, wakaamua kurudi nchini Marekani kuendelea na shughuli zao kama kawaida. Maisha yake yakabadilika, hayakuwa kama yalivyokuwa kipindi cha nyuma.

Japokuwa alikuwa na furaha tele lakini tatizo moja ambalo lilimfanya kukosa raha katika maisha yake ni juu ya afya yake tu. Alijitahidi kuwaona wataalamu mbalimbali, hakukuwa na mtu aliyemtibu hivyo kubaki hivyohivyo.

Siku zikaendelea kukatika, miezi ikakatika, baada ya miezi sita ya ndoa, mkewe, Katty akaanza kulilia mtoto. Huo ulikuwa mtihani mkubwa kwake, kama kufanya mapenzi, walifanya, tena kwa nguvu zote, kwa nini mtoto hakupatikana?

Hali hiyo ikampa mawazo mazito Dylan, yeye alilijua tatizo lakini mkewe hakujua kitu chochote kile. Kazi yake kubwa kwa kipindi hicho ikawa ni kumfariji tu kwamba muda ukifika, Mungu atawapa mtoto, kwa kipindi hicho walitakiwa kuendelea kusubiri.

“Tatizo nini mume wangu?” aliuliza Katty.

“Hata mimi sijui mke wangu.”

“Kama vipi tukamuone daktari...” alishauri Katty.

“Unahisi tunaweza kuwa na tatizo?”

“Nahisi itakuwa hivyo...”

Hicho ndicho walichotakiwa kufanya hasa katika hali kama hiyo. Kesho yake walikuwa katika Hospitali ya Marie Stopes ambapo wakakutana na daktari wao, Fabian na kumueleza tatizo lao.

“Poleni sana, ila hali kama hiyo inawatokea watu wengi, ngoja niwafanyie vipimo,” alisema Dk. Fabian na hivyo kuanza kazi ya kuwafanyia vipimo.

Muda wote Dylan alikuwa na mawazo tele, moyo wake ulimuuma mno, hakuamini kama bilionea kama yeye ndiye aliyekuwa akipitia maisha hayo. Mbele yake aliiona aibu kubwa, kitendo cha kushindwa kumpa mimba mke wake kilimfanya kuona kwamba siku yoyote ile angeweza kugundulika kile alichokuwa akikifanya kitandani.

Baada ya daktari kuwafanyia vipimo na wiki moja iliyofuata, wakafuata matokeo ya vipimo vyao na kuonekana wote wapo vizuri, hapakuwa na mtu yeyote aliyekuwa na tatizo lolote lile.

“Unasema kweli daktari?”

“Ndiyo Dylan, hakuna mwenye tatizo kabisa,” alijibu Dk. Fabian,

Wakaondoka mahali hapo huku daktari akiwataka kufika hospitalini hapo mara kwa mara kwa ajili ya kupewa ushauri juu ya kitu walichotakiwa kufanya.

Hilo wala halikuwa tatizo, mara kwa mara walifika mahali hapo kama walivyokuwa wakiambiwa, pamoja na hali yote hiyo, matokeo hayakuweza kubadilika, hali ilikuwa ileile kwamba mimba haikupatikana.

“Sasa tatizo litakuwa nini?” aliuliza Katty.

“Hata mimi sifahamu! Au twende sehemu za maombezi..”

“Labda, inawezekana kuna tatizo.”

Wakawa watu wa kwenda kanisani, huko, wakafanyiwa maombezi lakini bado hali iliendelea kuwa vilevile. Waliishi maisha ya majonzi, muda mwingine Katty alikuwa mtu wa kulia tu.

Siku nyingine hakuwa akizungumza na mumewe, hasira zilimkaba kooni na muda mwingi alikuwa akimlaumu Mungu. Kazi yao kubwa ilikuwa ni kubadilisha hospitali, kote huko, matokeo yaliendelea kubaki vilevile lakini Dylan alifahamu nini lilikuwa tatizo.

“Hivi siku akinigundua, itakuwaje?” alijiuliza Dylan.

“Nafikiri itakuwa mwisho! Mungu wangu, nitaishi maisha haya mpaka lini? Ngoja nimuone daktari, nahisi kuna kitu natakiwa kufanya,” alisema Dylan.

Siku hiyo hakutaka kurudi nyumbani mapema, alichokifanya ni kupitia hospitalini ambapo huko akaonana na Dk. Fabian na kuanza kuzungumza naye. Hakutaka kumficha, alijiweka wazi kila kitu kilichokuwa kikiendelea katika maisha yake.

“Ooppss...” alishusha pumzi nzito daktari.

“Ndiyo hivyo! Ninahitaji msaada wako,” alisema Dylan.

“Unafikiri nitakusaidia vipi?”

“Nataka tufanye kitu kimoja...”

“Kipi hicho...”

“Tupandikize mbegu za kiume katika yai la mke wangu,” alisema Dylan.

“Mbegu zako?”

“Hapana! Za mtu mwingine...”

“Mmh!”

“Nini sasa?”

“Nahisi inaweza kuleta matatizo baadaye...”

“Matatizo gani?”

“Huyo mtu akitoa siri...!”

“Sitaki ajue hizo mbegu zinakwenda wapi, iwe siri, nitamlipa dola milioni moja,” alisema Dylan.

“Kweli?”

“Ndiyo! Haina jinsi, nataka kumuona mke wangu akiwa na furaha siku zote katika maisha yake,” alisema Dylan.

Hakuwa na jinsi, kitu pekee alichokihitaji kwa wakati huo ni kumuona mke wake akiwa na furaha. Alijua kwamba jambo alilotaka kulifanya lilikuwa na hatari lakini hakujali, alizihitaji hizo mbegu za kiume kwa gharama zozote zile.

Alichokifanya ni kumuachia jukumu hilo Dk. Fabian ambaye kazi yake kubwa ilikuwa ni kumtafuta mtu ambaye angeweza kuifanya kazi hiyo, mwanaume mwenye sura nzuri ili mtoto atakayezaliwa basi awe na sura nzuri.

Kazi hiyo ikaanza mara moja, alichokifanya Dk. Fabian ni kuwatafuta vijana ambao waliingia mtaani na kumpata Mike ambaye walizungumza naye na kumpeleka hospitali pasipo kumwambia kwamba lengo la yeye kuwa mahali hapo ni kwamba mbegu zake zilikuwa zikihitajika sana.

“Kwa hiyo ishu ni kutoa mbegu tu?” aliuliza Mike.

“Ndiyo! Utapata dola milioni moja...”

“Kweli?”

“Ndiyo!”

“Hakuna kingine?”

“Hakuna!”

Kwake, kwa umasikini aliokuwa nao wala halikuwa tatizo, lilikuwa jambo dogo sana. Kutoa mbegu hizo huku akiingiza dola milioni moja ambazo kwa fedha za Kitanzania ilikuwa ni zaidi ya bilioni mbili, ilikuwa ni bahati mno.

Alichoambiwa ni kuingia ndani ya chumba kimoja kilichokuwa na televisheni, akapewa chombo na kisha kuwashiwa televisheni hiyo na kuwekewa filamu ya utupu huku akitakiwa kujichua.

Akaanza kazi huku akiwa peke yake. Dakika tano nyingi, akafanikiwa kutoa mbegu zake ambazo zilichukuliwa na kuwekwa kwenye mashine maalumu na kutakiwa kuondoka mahali hapo huku akiambiwa kwamba kila kitu kilichoendelea, kiwe siri, asijue mtu yeyote yule. Akakubaliana nao. Ndani ya saa tatu, kiasi hicho cha fedha kaingizwa katika akaunti yake.

****

“Nimeanza kusikia kizunguzungu mpenzi,” alilalamika Katty, ilikuwa ni saa sita usiku.

“Kuna nini tena mpenzi wangu?” aliuliza Dylan huku akionekana kuwa na wasiwasi.

“Sijui! Tumbo linaniuma, nisaidie, tumbo linaniuma na nasikia kizunguzungu, nisaidie mume wangu,” alipiga kelele Katty.

Hakukuwa na kitu kingine cha kufanya zaidi ya kumchukua mkewe, Katty, akambeba na kumpeleka ndani ya gari lake na kuanza safari ya kuelekea katika Hospitali ya Marie Stoppes Medical Center.

Njiani, bado Katty alikuwa akilalamika kwa maumivu huku kile kizunguzungu kikiongezeka kadiri dakika zilivyokwenda mbele. Dylan alichanganyikiwa, aliendesha gari kwa kasi ya ajabu mpaka walipofika katika hospitali hiyo ambapo harakaharaka akawaita manesi ambao wakafika mahali hapo na kumpakiza kwenye machela na kuanza kuisukuma kuelekea nani.

Dylan alikuwa akifuatilia kwa nyuma, alionekana kuchanganyikiwa, hakujua tatizo lilikuwa nini mpaka mke wake kuwa kwenye tatizo kubwa namna ile. Machela ile ikaingizwa katika chumba kilichoandikwa Theatre kwa mlangoni na yeye kuambiwa kubaki mahali hapo.

“Nataka niende na mke wangu,” alisema Dylan.

“Hapana...unatakiwa kubaki hapa,” alisema nesi.

“Nesi...nesi, ninampenda mke wangu, ninataka kuwa karibu naye...” aliendelea kusema Dylan huku akionekana kuchanganyikiwa mno, ugonjwa wa ghafla wa mkewe ulimuweka katika hali mbaya mno.

Hakuruhusiwa kuingia ndani ya chumba hicho, alitakiwa kubaki mahali hapo huku manesi wale wakienda na Katty ndani ya chumba kile. Huku nje, Dylan alibaki akiwa ametulia, muda wote alionekana kuwa na mawazo. Manesi walipokuwa wakitoka nje, aliwang’ang’ania na kutaka kujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea.

“Kuna nini? Nini kimemtokea mke wangu?” aliuliza Dylan huku akionekana kuchanganyikiwa.

“Hakuna kitu, subiri, daktari atakwambia kila kitu,” alisema nesi.

“Atapona?”

“Utaambiwa, subiri hapo,” alisema nesi huyo, hakutaka kubaki mahali hapo kwa kuogopa maswali mengi, huyo akaondoka zake.

Dylan alibaki mahali hapo huku akiwa na mawazo tele, alijiinamia chini, alionekana kuwa na wasiwasi mno, wala haukupita muda mrefu, mlango ukafunguliwa na nesi mwingine kutoka, akasimama na kumdaka na kumuuliza maswali mengine lakini nesi huyo hakutaka kujibu swali lolote lile.

Baada ya dakika chache, Dk. Fabian akatokea mahali hapo huku akiwa kwenye mwendo wa kasi, Dylan alipoyainua macho yake, wakagonganisha macho na daktari huyo kumkonyeza, akaachia tabasamu kisha kuingia ndani ya chumba kile.

Huo ndiyo ulikuwa mpango waliotaka kufanya, Dylan hakutaka kukosea, alijua siku za hatari za mke wake kushika mimba hivyo alihakikisha siku hiyo anafanya kitu kimoja kikubwa.

Kwanza akamuwekea madawa ya usingizi ambayo yangemfanya kusikia maumivu ya tumbo kwa mbali na kuhisi kizunguzungu na mwisho wa siku kupoteza fahamu. Hilo ndilo lililofanyika, wakati amejisikia kizunguzungu, akapoteza fahamu ili Dk. Fabian afanye kazi yake ya kupandikiza mbegu za kiume katika mwili wa Katty.

Hilo lilifanyika kwa siri, ni Dk. Fabian na daktari mwenzake, Dk. Alexander ndiyo waliojua mchezo huo. Mara moja, tena kwa haraka sana kazi ikaanza kufanyika ndani ya chumba hicho.

Dylan alikaa nje ya chumba kile, alijiona kuwa na mafanikio makubwa, alimshukuru Mungu kwa kufanikisha mpango huo, kazi kubwa ilibaki kwa madaktari hao ambao walimuongezea nusu kaputi kitandani pale.

Baada ya saa moja, kila kitu kikawa tayari, madaktari hao wawili wakatoka, kitu cha kwanza baada ya kuonana na Dylan nje ya chumba hicho ni kuanza kumpongeza na kumwambia ainge ndani ya chumba kile.

“Tumefanikiwa...” alisema Dk. Fabian.

“Kweli?”

“Asilimia mia moja, tumefanikiwa!”

“Asante Mungu, siamini!”

“Amini sasa, imekuwa kazi nyepesi mno!”

Wakapongezena, baada ya saa mbili, Katty akarudiwa na fahamu, mtu wa kwanza kabisa kumuona ndani ya chumba hicho alikuwa mume wake. Japokuwa ilikuwa ni saa nane usiku lakini mwanaume huyo hakulala, alipomuona mkewe amefumbua macho, uso wake ukaonyesha tabasamu pana.

“Mume wangu! Nini kilitokea?” aliuliza Katty huku akimwangalia Dylan usoni.

“Sijui! Ila madaktari wamekupima wamegundua kwamba kizunguzungu kimesababishwa na akili yako kuchoka, umefanya kazi mfululizo,” alijibu Dylan bila kupepesa macho pembeni, alitaka kuaminika zaidi.

Hata madaktari walipoingia, majibu yao yalikuwa yaleyale kwamba alifanya kazi kwa kipindi kirefu hivyo alichoka sana hali iliyompelekea kusikia kizunguzungu.

Saa tisa usiku, akaruhusiwa na kurudi nyumbani.

Usiku wa siku hiyo, ulikuwa ni wa mahaba mazito, Dylan hakutaka kuichezea nafasi hiyo, akaanza kumpapasa mkewe kitandani na mwisho wa siku wakajikuta wakiwa kwenye dimbwi la mahaba na hatimaye kuanza kuvuana nguo, kilichofuatia ni sauti za mahaba huku Dylan akiwa makini sana katika kucheza na kifaa kile cha bandia.


Dalili ya kwanza kabisa aliyoisikia baada ya wiki mbili ni kutapika, alijisikia uchovu mwingi, hakujua tatizo lilikuwa nini. Alichanganyikiwa, alihisi kwamba alikuwa akiumwa ugonjwa fulani wa hatari.

Kizunguzungu kikampata, muda mwingi akawa mtu wa kulala tu. Hakutaka kumsubiri mume wake, hapohapo akampigia simu na kumwambia alivyokuwa akijisikia.

“Mpigie simu daktari aje..” alisema Dylan.

Hicho ndicho alichokifanya, akachukua simu na kumpigia daktari wa familia na kumwambia kilichokuwa kikiendelea, Ndani ya dakika kadhaa, daktari huo akafika nyumbani hapo na kumfanyia vipimo.

Katty alikuwa pembeni, alikuwa akisubiri majibu, alitaka kujua tatizo lilikuwa nini. Moyo wake ulichanganyikiwa, alikumbuka vilivyo kwamba wiki mbili zilizopita alipata tatizo kama hilo, akahisi mwili wake ulikuwa na matatizo makubwa, hivyo alichokifikiria ni kwenda kuuchunguza mwili mzima.

“Kuna tatizo gani dokta?” aliuliza Katty.

“Siamini macho yangu!”

“Kuna nini?”

“Hebu njoo uone...” alisema daktari, Katty akasogea na kuanza kuangalia. Akamuonyeshea matokeo.

“Sielewi chochote, ndiyo nini?”

“Una mimba...”

“Unasemaje?” Katty aliuliza huku akionyesha mshtuko wa waziwazi.

“Una mimba, ndivyo kipimo kinavyonionyesha,” alisema daktari yule.

Katty akachanganyikiwa kwa furaha, hakuamini kile alichokisikia, hapohapo akajikuta akisimama na kumkumbatia daktari kwa furaha. Alibaki akipiga kelele kama chizi ndani ya nyumba hiyo, alikimbia huku na kule, alipagawa, akashindwa hata kumtaarifu mumewe.

“Asante Mungu! Asante Mungu!” alisema Katty, hapo ndipo akakumbuka kumpigia simu mume wake, akachukua simu yake na kumpigia.

“Mpenzi...” aliita mara baada ya simu kupokelewa.

“Kuna nini? Si unaumwa? Mbona unaonekana una furaha!”

“Nimemuita daktari..”

“Ikawaje?”

“Huwezi kuamini!”

“Kuna nini? Mbona unaniweka roho juu?”

“Nina mimba...nina mimba mume wangu...”

Dylan hakutaka kuzungumza suala hilo kwenye simu, alichokifanya ni kukata kisha kutoka ofisini mwake. Yeye mwenyewe alichanganyikiwa, hakuamini kama kile kitu alichokifanya yeye na madaktari kingeweza kufanikiwa kwa kiasi hicho.

Akaingia ndani ya gari, alikuwa na furaha tele na siku hiyo aliendesha gari kwa tahadhali kubwa, aliogopa kupata ajali na kufa pasipo kumuona mkewe akiwa mjauzito.

Alipofika nje ya nyumba yake, hata kabla geti halijafunguliwa, tayari aliteremka na kuingia kwa kutumia geti dogo. Mlinzi alibaki akimshangaa, hakujua bosi wake alikuwa na nini. Moja kwa moja akaingia ndani ambapo bado alimkuta mke wake akiwa na furaha na kuwapigia simu marafiki zake.

“Mke wangu...” aliita Dylan.

“Mume wangu! Nina mimba..” alisema Katty, hapohapo akamsogelea mumewe na kumkumbatia kwa furaha.

“Siamini! Dokta! Kweli mke wangu ana mimba?” aliuliza Dylan huku akimwangalia daktari ambaye bado alikuwa mahali hapo.

“Ndiyo! Mkeo ana mimba, nimempima.”

“Una uhakika?”

“Asilimia mia moja!”

Jibu hilo tu lilitosha kumfanya Dylan kumng’ang’ania mke wake kwa nguvu, hakutaka kumuachia mikononi mwake. Hatimaye alifanikiwa kile alichokuwa amekipanga.

*****

Mike alijiona kuwa bilionea mkubwa, hakuamini kama kitendo chake cha kutoa mbegu kwa ajili ya mtu asiyemfahamu kingemfanya kuwa tajiri kiasi hicho. Muda wote alikuwa mtu mwenye furaha, katika maisha yake yote aliishi maisha ya kimasikini mno, hakuamini kama muda huo naye alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa na fedha.

Kichwa chake kilikuwa na akili kubwa, alijua kwamba hakuwa na fedha kabla na alimuomba sana Mungu apate fedha, na kweli katika kipindi hicho alipata kiasi kikubwa cha fedha hivyo jambo la kwanza kabisa alilolifikiria ni kuanzisha biashara.

Biashara ambayo ilikuja kichwani mwake ni kuwa mfanyabishara wa mafuta. Hakukuwa na kazi nyingine ambayo aliiona kuwa na faida kubwa na ambayo ilifanywa na watu wenye kiu ya kutaka kupata mafanikio kama hiyo.

Kitu cha kwanza alichokifanya ni kuonana na Bwana Peters Brown aliyekuwa mkurugenzi wa kampuni ya mafuta ya Oilcom na kuanza kuzungumza naye. Mazungumzo hayo yalichukua saa moja, lengo kubwa la mazungumzo hayo na mzee huyo ni kumwambia kwamba naye alitaka kuweka hisa katika kampuni hiyo, hata kama angepata kiasi kidogo cha fedha, kwake ingemsaidia.

“Kiasi gani?” aliuliza Bwana Peters.

“Nataka niweke dola laki tano...” alisema.

“Una uhakika utapata faida?”

“Kwa nini isiwezekane?”

“Ngoja nikwambie kitu kimoja!”

“Kitu gani?”

“Hii kampuni inakaribia kufilisika....”

“Unasemaje?”

“Ndiyo hivyo! Kama kweli unajiona unaweza kufanya biashara hii tena ukapata faida, basi nikuuzie kabisa,” alisema mzee huyo.

“Kiasi gani?”

“Dola milioni tano!”

“Mbona nyingi hivyo na wakati biashara yenyewe inakaribia kufilisika?” aliuliza Mike huku akionekana kushangaa.

“Ni kwa sababu ina faida.”

“Kama ina faida, kwa nini unataka kuachana nayo?”

“Ni mambo mengi sana, kubwa ni kwamba nataka nianzishe biashara nyingine, hii ya kusafirisafiri kwenda Uarabuni, nimechoka,” alisema mzee Peters.

Walizungumza mambo mengi kuhusu biashara hiyo. Kwa Mike, aliona kwamba ilikuwa biashara nzuri ambayo kama angeamua kuifanya basi ingekuwa na faida kubwa. Alichokifanya ni kuzungumza na mzee huyo na kumwambia kwamba lingekuwa jambo zuri kama angemuuzia kwa kumpa kiasi kidogo cha fedha na baadaye kummalizia.

“Hakuna tatizo....kikubwa uaminifu..”

Hapo ndipo alipoanza kufanya biashara hiyo ya mafuta, ilikuwa ni biashara ngumu kwa kipindi cha kwanza lakini Mike hakutaka kukata tamaa. Alisafiri huku na kule, alitafuta masoko na hatimaye ile kampuni ya Oilcom ambayo ilikuwa ikielekea kufilisika ikaanza kusimama.

Hakutaka kulegea, kila siku ilikuwa ni lazima kuwalazimisha wafanyakazi wake kufanya kazi kubwa usiku na mchana huku akipunguza gharama za uuzaji wa mafuta hayo kitu kilichomfanya kufanikiwa kwa haraka mno.

Alichukiwa na wauzaji wengine wa mafuta lakini hakujali, alichokuwa akikiangalia ni kupata fedha ya haraka kwani bado alikuwa na deni kubwa kutoka kwa Bwana Peters.

Mwaka wa kwanza ukakatika, wa pili ukaingia na hatimaye akafanikiwa kulipa deni lililobaki na hivyo kuanza kuingiza fedha katika akaunti yake. Biashara ilichanganya, akaingiza kiasi kikubwa cha fedha, hakuwa mtumiaji, alijua kwamba ili uwe na utajiri mkubwa ilikuwa ni lazima uwe na nidhamu ya fedha katika matumizi, na hicho ndicho alichokifanya.

Alianza chini kabisa lakini kadiri siku zilivyozidi kwenda mbele na ndivyo alivyozidi kufanikiwa zaidi. Hakulala usiku kucha, kila siku ilikuwa ni kufuatilia mauzo, yalikwendaje, wapi yaliishia na kwa namna gani alitakiwa kuyaendelea kutoka pale yalipogotea.

Baada ya kupita miezi sita, ndipo alipoamua kuangalia akaunti yake ilikuwa na kiasi gani kwani kwa kipindi kirefu hakuwa amefanya hivyo. Alipoangalia, hakuamini macho yake, kulikuwa na zaidi ya dola bilioni mbili, hakuamini, akapiga magoti chini na kumshukuru Mungu kwa kile alichokiona.

“Na mimi ni bilionea?” alijiuliza huku akionekana kushangaa.

Huo ulikuwa mwanzo, mwanzo wa kujinyima mpaka kufikia malengo yake. Hakuishia hapo, aliendelea kupambana kila siku, alitamani kuingiza kiasi kikubwa cha fedha zaidi na zaidi.

Mara kwa mara alikuwa mtu wa kwenda katika nchi za Kiarabu, huko, alikutana na wafanyabiashara wenzake na kuzungumza mengi kuhusu biashara hiyo. Alijiona kuwa mtu mwenye bahati kubwa, wakati mwingine, hakuamini kama kile kilichokuwa kikitokea kilitokea katika maisha hayahaya na si ndoto.

“Umependeza...” alisema msichana mmoja, alikuwa Mwarabu mwenye sura nzuri, alikuwa akimwambia Mike.

“Asante sana...”

“Umetoka wapi?”

“Marekani!”

“Karibu sana, naitwa Aisha, ni mwenyeji wa hapa Kuwait...” alisema msichana huyo huku akimpa mkono Mike.

Kipindi hicho alikuwa nchini Kuwait, alikwenda huko kwa kuwa kulikuwa na mazungumzo mazito kuhusu biashara ya mafuta aliyokuwa akifanya na Waarabu nchini humo.

Hakutaka kumtuma mwakilishi wake, kwa kuwa ulikuwa ni mkutano mkubwa alitaka kwenda yeye mwenyewe. Huku wakiwa katika mkutano huo ndipo alipokutana na msichana huyo aliyejitambulisha kwa jina la Aisha.

Alikuwa mzuri wa sura, alivalia nguo ya heshima na kichwani alivalia hijabu ya bluu, machoni alivalia miwani, kila alipotembea, alitembea kwa madaha na kuwaacha wanaume wengine mdomo wazi.

Huyo alikuwa mtoto wa mfalme wa Kuwait Sabah Al-Ahmad, alikuwa msichana mrembo mno ambaye alipendwa na wanaume wengi huko Kuwait. Japokuwa baba yake ndiye alikuwa kiongozi wa nchi hiyo lakini hakutaka kuishi kama mtoto wa mfalme bali alitaka kuishi kama mtu wa kawaida tu.

Alikuwa mfanyakazi katika Kampuni ya Mafuta ya Al Jazeebablon iliyokuwa ikifanya kazi ya kusambaza mafuta katika nchi mbalimbali duniani. Katika maisha yake yote mpaka kipindi hicho, Aisha hakuwahi kumjua mwanaume kwani muda mwingi alikuwa msichana wa kuchungwa, alipokwenda, alichungwa, hakutakiwa kusogeleana na mwanaume yeyote yule.

“Ila hata wewe umependeza....”

“Kweli?”

“Ndiyo! Hongera sana! Halafu sasa....”

“Halafu nini?” aliuliza Aisha huku akiachia tabasamu pana lililomvuruga kabisa Mike. Akameza mate.

“Au basi...”

“Hapana! Niambie, halafu nini?” aliuliza msichana huyo. Tayari hali ya Mike ikabadilika. Mwili ukaanza kumsisimka kupita kawaida. Watu wote waliokuwa mahali hapo, wakabaki wakiwaangalia wawili hao, nao wakajisahau kabisa kama walikuwa katika meza ndefu, kikaoni, tena kulikuwa na watu zaidi ya ishirini.

Wakabaki wakiangaliana tu.


Muda wote Dylan na mkewe walionekana kuwa na furaha tele, hawakuamini kilichokuwa kikiendelea kwamba mwanamke huyo alishika ujauzito ambao kadiri siku zilivyokuwa zikizidi kwenda mbele, tumbo lake likaanza kuonekana.,


Dylan hakuamini kama mwisho wa kila kitu, mkewe angepata ujauzito na hivyo yeye kuitwa mwanaume kamili kama ilivyokuwa wengine. Kila alipopita, mikono yake aliitanua, ofisini kwake, kila wakati alikuwa akiwaambia wafanyakazi wenzake ni jinsi gani alikuwa na furaha na jinsi alivyohangaika kumfanya mke wake kushika ujauzito huo.


Hakumfikiria mwanaume ambaye alizitoa mbegu zake kwa ajili ya mke wake, alichokifikiria kwa wakati huo ni mkewe tu, tena kwa kujitapa kwamba watoto walikuwa wake.


Kwa Katty, muda wote alikuwa na furaha hakutaka kutoka nyumbani kwake, kila siku alibaki ndani, alihisi kwamba anaweza kupata ajali na kufariki, alijichunga na kadiri siku zilivyokuwa zikienda mbele, Marekani nzima wakajua kwamba mke wa bilionea Dylan alikuwa mjauzito.


“Mimi kidume Christina, nilikwambia, ukabisha,” Dylan alimwambia ndugu yake wakati wakiongea kwenye simu.


“Safi sana, umefanya kazi kubwa, tunahitaji kupata watoto wetu sasa,” alisema Christina huku kwa sauti yake tu, ilionyesha ni jinsi gani alikuwa na furaha.


Siku zikaendelea kukatika, Dylan akashindwa kuvumilia, alichokifanya ni kumnunulia mkewe zawadi ya gari la thamani aina ya Buggati ambalo hilo alitaka alitumie kipindi alichokuwa akienda hospitalini.


“Nashukuru sana mume wangu! Unanifanya nijisikie kupendwa sana,” alisema Katty pasipo kufahamu kilichotokea nyuma ya pazia.


Mimba tu ikaanza kuwaweka pamoja na kwa ukaribu mkubwa. Dylan akawa mtu wa kuwahi kurudi nyumbani, kuliona tumbo la mkewe, ilimpa furaha kubwa.


“Daktari amesemaje?” aliuliza Dylan.


“Amesema nina mapacha! Wa kike na wa kiume.”

“Unasemaje?”

“Nina mapacha mume wangu!”


Dylan hakuamini, hapohapo akamkumbatia mkewe, akashindwa kuvumilia, machozi ya furaha yakaanza kumtiririka mashavuni mwake. Shukrani zake zote zilikuwa kwa Dk. Fabian ambaye ndiye aliyefanikisha suala zima la upachikaji wa mbegu katika yai la mkewe.


“Nashukuru kwa kila kitu!”


“Asante na wewe pia! Hakika najisikia faraja sana kuona zoezi langu limefanikiwa,” alisema Dk. Fabian huku akiwa na furaha mno.


Baada ya miezi tisa, Katty akaanza kujisikia uchungu wa kuzaa. Siku hiyo, Dylan alikuwa nyumbani kwake, ilikuwa ni saa sita usiku. Wakati mkewe akilalamikia uchungu, tayari gari lilikuwa tayari nje kwani alijua kwamba kitu kama hicho kingetokea kutokana na muda kufika.


Alichokifanya ni kumbeba na kumpeleka ndani ya gari na safari ya kuelekea hospitalini kuanza. Njiani, alikuwa na furaha tele. Hawakuchukua dakika nyingi, wakafika ambapo manesi wakaleta machela na yeye kuanza kuifuata kule manesi walipokuwa wakiisukumia, walipofika katika chumba kilichoandikwa ‘Labour’ akatakiwa kusubiri kwenye viti vilivyokuwa nje ya chumba hicho.


Huku nje, alikuwa na presha kubwa, muda wote alikuwa amesimama, alitembea huku na kule, alitaka kusikia watoto wakilia ndani ya chumba hicho. Watu wote waliokuwa katika eneo hilo walibaki wakimwangalia, walimfahamu, alikuwa bilionea mkubwa Marekani, utajiri ambao aliachiwa na baba yake aliyekuwa amezeeka na hivyo kuhitaji msimamizi.


Baada ya dakika arobaini na tano, akajikuta akianza kurukaruka kwa furaha, hakuamini hata kidogo kile alichokisikia ndani ya chumba hicho. Sauti za watoto zikaanza kusikika. Akajikuta akitoka mbio na kuwakumbatia madaktari waliokuwa mahali hapo, tena kwa zamu. Kile kilichotokea, kilidhihirisha kwamba yeye naye alikuwa mwanaume rijali.


****


Walibaki wakiangaliana, macho yao tu yalionyesha kila kitu kilichokuwa kikiendelea mioyoni mwao. Watu wengine walibaki wakiwaangalia Mike na msichana Aisha, hawakuonekana kuwa mahali hapo, mawazo yao yalikuwa yamehama na yalikwenda sehemu nyingine kabisa.


Mwenyekiti wa mkutano huo akajikoholesha kama njia mojawapo ya kuwaambia watu hao kwamba walitakiwa kuacha kile kilichokuwa kikitokea kwao na wamsikilize yeye.


Hiyo ilisaidia, Mike akamgeukia mwenyekiti huyo lakini muda wote macho yake yalikuwa kwa msichana huyo. Siku hiyo, tena kwenye kikao hicho kazi ilikuwa ni kuangaliana kwa zamu tu.


Mapenzi mazito yakawaingia wote wawili, hawakuamini kama ingechukua muda mfupi kiasi hicho mpaka macho yao kuzoeana. Mkutano uliendelea, ulipomalizika, Mike akashindwa kuvumilia, akamfuata msichana huyo.


“Unaniangalia sana....” alisema Aisha.


“Kwa sababu u mzuri sana, siamini kama duniani kungekuwa na msichana mrembo kama wewe,” alisema Mike, macho yake tu yalionyesha ni kwa kiasi gani alikubaliana na uzuri wa msichana huyo.


“Kweli?”

“Ndiyo!”


“Asante!”


Aisha hakutaka kukaa sana kuzungumza na Mike, alizijua sheria za nchi hiyo, haukutakiwa kupendana na kuishia njiani, kama kweli mlipendana basi ilikuwa ni lazima kuoana na si kuchezeana, sheria nyingine ni kwamba hamkutakiwa kufanya ngono mpaka pale mtakapoona, vinginevyo, mkigundulika mnapigwa mawe hadharani mpaka kufa.


“Aisha...” aliita Mike. Aisha akageuka.


“Unasemaje?”

“Una macho mazuri sana, naomba unitafute...” alisema Mike, akampa kikaratasi kilichokuwa na namba yake na kisha kila mmoja kuondoka.


Hotelini, bado Mike alikuwa amechanganyikiwa. Sura ya mtoto wa Kiarabu ilimchanganya mno, hakuamini kama kweli angekutana na msichana huyo nchini Kuwait.


Usiku hakulala, alibaki akimfikiria msichana huyo mrembo kiasi kwamba akajisahau kabisa na mawazo kuhusu ndoa yakaanza kumuandama. Kwa sababu alimpa namba ya simu, alichokuwa akikisikilizia kipindi hicho ni kupigiwa simu tu.


Ilipofika saa tatu usiku, simu yake ikaanza kuita, hakuamini, namba ilikuwa ngeni hivyo harakaharaka akaichukua na kuipokea.


“Aisha...” alijikuta akiita baada ya kupokea.


“Umejuaje?”

“Hakuna mwenye namba yangu ambaye anaweza kupiga muda huu zaidi yako mrembo,” alisema Mike huku akiachia tabasamu pana kana kwamba msichana huyo alikuwa mbele yake.


“Mmmh! Aya! Niambie unataka kuniambia nini?” aliuliza Aisha.


“Nataka twende sehemu, tukakae na kuzungumza,” alijibu Mike.


“Sehemu gani?”

“Yoyote ile ya siri! Tukutane kisiri na tuzungumze...” alisema Mike.


“Mmh! Si Marekani hapa, ni Kuwait, hilo jambo haliwezekani,” alisema msichana Aisha.


“Kwa hiyo inakuwaje?”


“Labda tukutane sehemu nyingine.”

“Wapi?”

“Dubai! Huko kidogo sheria hazibani!” alijibu msichana huyo.


“Hakuna tatizo! Nataka twende kesho!”

“Ila si kuna mkutano mwingine!”

“Achana nao! Wewe ni muhimu kuliko hata huo mkutano!” alisema Mike. Aisha akacheka kidogo, wakakubaliana na simu kukatwa.


Kilichofuata ni Mike kuwa na presha kubwa ya kukutana na msichana huyo huku akijua kwamba watakapofika Dubai, hakuna sehemu yoyote ambayo wangekutania zaidi ya hotelini ambapo huko angemaliza kila kitu.


“Lazima...lazima, sijawahi kumpata Mwarabu...lazima,” alijisemea huku akivua nguo zake kwa ajili ya kulala. Hata usingizi haukumpata kwa wakati, kila wakati alimfikiria Aisha tu.


ITAENDELEA

No comments:

Featured Post

 SOMA SIMULIZI ZENYE KUSISIMUA HAPA A. UTAJIRI WENYE UCHUNGU     UTAJIRI WENYE UCHUNGU-1     UTAJIRI WENYE UCHUNGU-2      UTAJIRI WENYE UCH...